Header Ads Widget

UWT WAMPONGEZA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO KWA WANANCHI

UWT WAMPONGEZA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO KWA WANANCHI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

JUMUIYA ya Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT),wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan, kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi.

Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Taifa Zainab Shomari amebainisha hayo leo Agost 26,2023 wakati wa ziara ya kukagua utelekezaji wa miradi ya maendeleo Kata ya Chamaguha na Kitangili Manispaa ya Shinyanga.
Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Zainab Shomari.

Amesema amefarijika kuona jinsi Rais Samia alivyotekeleza miradi mingi ya maendeleo kwa wananchi ikiwamo ya huduma za Afya, Elimu, Maji, Miundombinu ya Barabara pamoja na ujenzi wa Madaraja.

"Tuendeleeni kumuunga Mkono Rais wetu Samia kwa tunaona jinsi anavyotekeleza miradi mingi ya maendeleo ikiwamo na ujenzi wa miradi mikubwa ya kimkakati," amesema Shomari.
Daraja la Kitangili Manispaa ya Shinyanga.

Aidha,amewataka wanawake kote nchini kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani pamoja na uchaguzi Mkuu 2025.

Naye Mbunge wa Vitimaalumu Mkoa wa Shinyanga Santiel Kirumba, ametoa wito kwa wanawake kuchangamkia fursa za mikopo asilimia 10 ya Halmashauri ambayo hivi karibuni itaanza kutolewa na kuachana na mikopo umiza ambayo imekuwa ikiwarudisha nyuma kimaendeleo.
Mbunge wa Vitimaalumu Mkoa wa Shinyanga Santiel Kirumba.

Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Gasper Kileo, amewaomba Watanzania kuendelea kumuunga Mkono Rais samia katika utekelezaji wa maendeleo ikiwamo na suala la uwekezaji wa Bandari.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Gasper Kileo.
Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Zainab Shomari akikagua utekelazaji wa ujenzi wa daraja ambalo lina unganisha Kata Mbili za Chamaguha na Kitangili.
Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Zainab Shomari akikagua utekelazaji wa ujenzi wa daraja ambalo lina unganisha Kata Mbili za Chamaguha na Kitangili.
Daraja jipya la Kitangili.
Ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UWT Shinyanga Mjini ikiwekewa jiwe la Msingi.
Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Zainab Shomari akiweka Jiwe la Msingi ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UWT Shinyanga Mjini.
Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa Makamu wa UWT Taifa Zainab Shomari.
Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa Makamu wa UWT Taifa Zainab Shomari.
Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa Makamu wa UWT Taifa Zainab Shomari.
Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Zainab Shomari akipiga picha ya pamoja na wanawake wa Chamaguha akiwamo Mama Aisha Stima.
Picha ya pamoja zikiendelea kupigwa.

Post a Comment

0 Comments