Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waandishi wa Habari kutoka Vyombo Mbalimbali vya Habari nchini Tanzania wanatarajia kufanya ziara ya siku tano kuanzia Agosti 14,2023 Mkoani Mara kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 20 ya Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI - The U.S. President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR) nchini Tanzania.
Serikali ya Marekani na Serikali ya Tanzania ilianzisha Mpango wa PEPFAR mnamo mwaka 2003 baada ya Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush kutangaza Mpango wa Dharura wa Kukabiliana na UKIMWI.
Kupitia Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa cha Marekani (The U.S. Center for Disease Control -CDC) kupitia Amref Health Africa Tanzania wanatekeleza afua mbalimbali za afya mkoani Mara.
Sehemu ya Waandishi wa Habari kutoka Vyombo Mbalimbali vya Habari nchini Tanzania na wadau wa afya wakiwa katika picha ya pamoja leo Jumamosi Agosti 12,2023 kabla ya kuanza kufanya ziara Mkoani Mara kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 20 ya Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) nchini Tanzania.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464