Diwani wa kata ya Seke Bugolo Ferdnand Mpogomi akizungumza na wenyeviti wa vijiji wakiwa katika ofisi za kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) inayotekeleza mradi wa SGR ilipokuwa imejengwa zahanati ya kijiji cha Seke Ididi
Suzy Luhende Shinyanga press blog
Wananchi wa kijiji cha Seke Ididi kata ya Seke Bugolo halmashauri ya wilaya ya Kishapu wameiomba serikali iwajengee zahanati ya kijiji hicho ili kuondokana na changamoto ya kina mama wajawazito kujifungulia njiani kutokana na kufuata huduma za matibabu umbali wa kilomita saba.
Ombi hilo limekuja baada ya wananchi wa kijiji hicho kubomolewa zahanati yao waliyokuwa wameijenga na kuifikisha kwenye lenta kwa kutumia fedha walizokuwa wakichangishana ambapo baada ya kubomolewa zilijengwa ofisi za kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) inayotekeleza mradi wa SGR.
Wakizungumza na waandishi wa habari waliotembelea katika kijiji hicho leo akiwemo Phinius Mauma amesema wananchi wanapata changamoto sana wanapougua hasa watoto wadogo na kina mama wajawazito wanapohitaji huduma ya kujifungua, kwani kutokana na umbali wa hospitali wengi wao wamekuwa wakijifungulia njiani na wengine kuhatarisha maisha yao.
"Tunaishukuru sana serikali yetu kwa kutuletea mradi huu wa reli ya mwendo kasi, lakini tunaiomba itusaidie kutujengea zahanati yetu iliyobomolewa kwani tuliona kuna changamoto kubwa ndiyo maana tukaamua kuchangishana ili tuwe na hospitali karibu, na baada ya kampuni hii kuomba ijengwe hapa tukiahidiwa tutajengewa sehemu nyingine zahanati hii na tulipewa kiwanja kabisa,"amesema Mauma.
"Lakini mpaka sasa mradi huu unaelekea mwishoni hatujajengewa tunaona tu wenzetu wanaendelea na kazi zao, hivyo tunaona kama vile tumesahaulika kabisa ukiangalia na watu wameshakuwa wengi katika kijiji hiki lakini hakuna hata zahanati, tunaomba mama yetu mama Samia utuhurumie tunateseka tujengewe zahanati yetu iliyobomolewa"amesema Mauma.
Adija Makongolo mkazi wa kijiji cha Seke Ididi amesema "sisi wanawake tunapata changamoto sana pale tunapoumwa uchungu tunajifungulia njiani na tunapougua tunpata shida kufika hospitali kwa sababu ni mbali na hospitali yetu imeshabomolewa tuiombe serikali itusaidie,".
Choletha Sengelema amesema, tunamuomba mama mwenzetu mama Samia Rais wetu atusaidie sisi wanawake ndio wazazi ndio walezi, tunapotaka kujifungua tunapata shida ndio maana tukaamua tujinyime tuchangie ujenzi wa jengo la Zahanati ili tusisababishe magonjwa ya vistura maana tunashauliwa ukichelewa kujifungua unaweza kupatwa na vistura lakini ni miaka miwili toka jengo letu libomolewe hatujajengewa zahanati yetu"
Mwenyekiti wa kijiji cha Seke mjini Omary Abdalah kutokana na ujenzi wa SGR watu wamekuwa wengi wanahitaji huduma za afya, lakini hazipo hapa akiugua mtu inabidi apelekwe kupatiwa huduma katika kata zingine ambazo ziko mbali, wananchi walijichangusha wakajenga zahanati na kufikia kwenye lenta lakini illikuja ikabomolwana kuahidiwa kuwa tutajengewa sehemu nyingine lakini mpaka sasa kimya tu.
"Sisi tulikuwa tumepata eneo letu na mabati yalikuwa tayari yameandaliwa na hospitali ingekuwa imeshaanza kutumika lakini sasa kimya tunashindwa kuelewa ni kwa nini hatujengewi na huku tuliahidiwa kwamba tunajengewa kina mama wanajifungulia barabarani ukiangalia barabara zetu haziko vizuri za kuweza kuwafikisha kwa wakati kupatiwa huduma"amehoji mwenyekiti Abdalah.
Mwenyekiti wa kijiji cha Seke Ididi Raymond Masele amesema mradi wa SGR ulanzishwa kijijini hapo 2021 walikuwa tayari wameshajenga jengo la zahanati na kufikia kwenye lenta lakini mradi wa SGR ulikuja kuvunja jengo hilo tangu mwaka huo waliahidi watalipa zaidi ya Sh 10 mpaka leo hakuna huduma ya zahanati.
"Tunaomba tujengewe zahanati, tunamuomba mama yetu msikivu anayeiongoza awamu ya sita asikie kilio cha wana Ididi kwani tunafuata huduma ya matibabu umbali wa kilomita sita hadi saba ni shida hivyo tunaomba basi tujengewe ili wananchi wapate huduma karibu na kuepusha vifo vinavyoweza kusababishwa na umbali wa huduma ya matibau"amesema Masele
Diwani wa kata ya Seke Bugolo Ferdnand Mpogomi wananchi walikuwa wakitembea umbali mkubwa wakachanga fedha zao wakaanzisha ujenzi na mfuko wa jimbo ulitoa mifuko 75 baada ya kuanzishwa mradi huo wakalifanyia uthamini wa zaidi ya zaidi ya Sh 10 milioni na tayari eneo la zaidi ya heka tatu na mchanga wananchi walisomba na kutafuta mzabuni lakini hawaoni kinachoendelea.
"Kijiji hiki kulikuwa na tatizo la huduma za afya kina mama walikuwa wanaenda kupata huduma kijiji cha Wishiteleja kilomita zaidi ya sita wengine kwenda Bugoro wakaamua wao wenyewe wajichangishe na ofisi ya mbunge ikaleta mifuko ya saruji 75 na mabati baadae mradi wa SGR wakapenda na kujenga majengo yao tumefanya jitihada tukapata eneo la zaidi ya heka tatu, tunaomba serikali itusaidie na kutujengea zahanati hii ili kuokoa maisha ya wananchi"amesema Mpogomi.
"Tayari tulitafuta mzabuni ambaye alikuwa ameleta hadi vifaa vyake kwa ajili ya kuanza ujenzi lakini baada ya kuona kimya alibeba vifaa vyake na kuenda kufanya kazi sehemu nyingine baada ya kuuliza TRC walisema suala hilo lipo Tamithemi, tunaomba tujengewe zahanati kwani inaonekana fedha hizi zimepotea,tunamuomba Rais na waziri wa uchukuzi wasikilize kilio chetu, vijiji nane viko bega kwa bega na Rais,"amesema Mpogomi.
"Lakini pia kuna kisima cha maji kijiji cha Dulisi ambacho kimepitiwa na ujenzi wa Reli ambao ulijengwa kwa nguvu ya wananchi, na wananchi wanakitegemea hicho hicho, tukiambiwa mkandarasi atatujengea lakini mpaka sasa bado tunahitaji msaada wananchi wanapata shida wanashindwa hata kuagiza watoto kwa sababu eneo hilo la kisima magari yanapishana,"ameongeza Mpogomi.
Kwa upande wake meneja wa SGR kituo cha malampaka Christopher Lamshai amesema mpaka sasa hakuna taasisi ya serikali ambayo imeshalipwa na maelekezo kila mkurugenzi awasiliane na katibu mkuu wake ili waingie kwenye mchakato wa kujenga kwani kuna taasisi mbalimbali za kiserikali ambazo zimezulika bado hazijalipwa.
"Hivyo tutaendelea kuikumbusha wizara ili iweze kuwatekelezea mahitaji yenu ya zahanati, lakini lile la kisima hilo nitalifatilia mimi mwenyewe iki kujua tunafanya utaratibu gani ili wananchi waweze kuchimbiwa kisima sehemu nyingine,"amesema Lamshai.
Ferdinand Mpogomi akizungumzia kisima kilichopitiwa na ujenzi wa reli SGR ambapo ameiomba serikali kusikia kilio cha wananchi kuwajengea sehemu nyingine kisima hicho ambacho kinaweza kubomolewa wakati wowote
Ferdinand Mpogomi akizungumzia kisima kilichopitiwa na ujenzi wa reli SGR ambapo ameiomba serikali kusikia kilio cha wananchi kuwajengea sehemu nyingine kisima hicho ambacho kinaweza kubomolewa wakati wowote
Mwenyekiti wa kijiji cha Seke Ididi Raymond Masele akizungumza na kuiomba serikali isikie kilio cha wananchi waweze kujengewa Zahanati
Baadhi ya wananchi wakichota maji katika kisima cha maji hayo ambacho kinaweza kubomewa wakati wowote
Baadhi ya wananchi wakichota maji katika kisima cha maji hayo ambacho kinaweza kubomewa wakati wowote
Baadhi ya wananchi wakichota maji katika kisima cha maji hayo ambacho kinaweza kubomewa wakati wowote
Baadhi ya wananchi wakichota maji katika kisima cha maji hayo ambacho kinaweza kubomewa wakati wowote
Eneo ilipokuwa zahanati iliyojengwa kwanguvu za wananchi ambayo ilibomolewa na kujengwa ofisi za Kampuni ya china CCECC inayotekeleza mradi wa SGR