Wahitimu wa chuo cha sayansi ya afya Kahama wakijiandaa kuingia ukumbini.
Na Kareny Masasy,
Kahama
TAASISI binafsi zinazowekeza kwenye vyuo vinavyotoa taaluma mbalimbali zinazoshughulikia masuala ya afya kwa binadamu zimeshauri kuweka na kozi ambazo wataalamu wake wachache ili kuendana na soko la ajira.
Hayo yamesemwa leo tarehe 10/08/2023 na mgeni rasmi Mdoe Ibrahimu ambaye ni kaimu mkurugenzi wa mafunzo kutoka wizara ya afya akimwakilisha naibu waziri wa Afya Godwin Mollel kwenye mahafali ya saba katika chuo cha sayansi za afya Kahama (KACHS).
Ibrahimu amesema kuna vyuo 219 vinavyotoa taaluma ya masuala ya afya ambapo vyuo vya serikali ni 43 tu hivyo serikali imejitahidi kutoa ajira kwa waliohitimu ufamasia na utabibu lakini kuna changamoto za kozi zingine kama uungaji wa viungo vya mwili kama umepata ajali na afya ya akili wanahitajika wataalamu.
Ibrahimu amesema wahitimu wanaomaliza wakiwa wanasubiri ajira wajikite kwenye masuala mengine wakipata fursa wasikae tu mitaani na waendelee kuielimisha jamii na wakipata ajira waitumie vizuri wasiwe chanzo cha kukosa maadili.
“Wakufunzi nanyinyi muwafundishe namna ya uvaaji na kujiweka utakuta mtumishi wa afya kucha ndefu kapaka rangi, koti na suruali vimebana nywele mitindo ya siku hizi kama mwanamziki taaluma haitaki mambo hayo”amesema Ibrahimu.
Ibrahimu amesema suala la vyuo vya kati wanafunzi kupata mkopo kama vyuo vingine hilo lilijadiliwa bungeni na baadhi ya wabunge walitoa mapendekezo na serikali ililichukua hivyo utaratibu ukiwepo umma utajulishwa.
Mkurugenzi wa chuo hicho Yona Bakungile amewapongeza walimu kutoa mafunzo kwa wahitimu kwani mafunzo haya ya afya ni magumu na ukiona kijana kamaliza ni jambo la kumshukuru mungu kwani wapo walirudia mwaka jana walifeli,wapo waliougua na wapo waliokatiza masomo sababu ya ada.
“Ninyi wahitimu mkipata ajira muende mkawatumikie wananchi kwa kuisadia serikali na shule za sekondari zimejengwa kila kona zikimaanisha vyuo kupata wanafunzi hivyo aliomba serikali kuwapatia mkopo wanafunzi kwani wao hawapati ruzuku ikitokea mwanafunzi ameshindwa kulipa ada basi chuo hakina namna”amesema Bakungile.
Akisoma risala kwa niaba ya wahitimu Aloyce Mzaga amesema wameweza kumudu masomo hivyo wanaahidi kwa serikali pindi wakipata ajira kuitumia vyema taaluma hiyo ambapo wahitimu wa ustawi wa jamii, maendeleo ya jamii,tabibu na ufamasia ni 162.
“Chuo hicho
kilianza mwaka 2016 kinajikita katika
mafunzo yenye ubora na changamoto inayotukumba ni baadhi ya wanafunzi kukatiza masomo sababu
ya ada hivyo tunaiomba serikali kutupatia mkopo sisi wanafunzi tuliopo kwenye vyuo vya kati”amesema Mgaza.
Mkurugenzi wa chuo cha Sayansi na Afya Kahama Yona Bakungile akiongea siku ya Mahafali ya saba ya chuo hicho.
Mkuu wa chuo cha sayansi ya Afya Kahama Vivian Mpangalala akitambulisha wageni waalikwa siku ya mahafali chuo hicho.
Mgeni rasmi Mdoe Ibrahimu ambaye ni kaimu mkurugenzi wa mafunzo kutoka wizara ya afya akimwakilisha naibu waziri wa Afya. siku ya Mahafali ya saba katika chuo cha sayansi na Afya Kahama akitoa neno kwa wahitimu na kukishauri chuo hicho.
Mwanafunzi Aloyce Mgaza akiwa maabara ya kujifunzia kwa vitendo ambaye anahitimu.
Wanafunzi wa chuo wakiwa katika maabara ya kujifunza kwa vitendo.
Wanafunzi wa chuo cha sayansi na Afya Kahama wakimpima mmoja wa wateja aliyejitokeza kupimwa.
Wanafunzi wakisubiri kutoa maelezo kwa mgeni rasmi
Wanafunzi wakiwa maabara ya kujifunzia
Walimu wa chuo cha sayansi na Afya Kahama .
Wageni waalikwa katika mahafali ya chuo.