Suzy Luhende, Shinyanga press blog
Askofu wa kanisa la Pefa Daniel Kwilemba lililopo Zanzibar amewataka waumini wa kanisa la Jesus Cares Church (JCC) kupendana na kushirikiana kwa pamoja katika kuifanya kazi ya Mungu kwa sababu yeye anawapenda wampendao.
Hayo ameyasema hivi karibuni kwenye ibada ya kumshukuru Mungu kwa kutimiza mwaka mmoja tangu kanisa hilo lianzishwe, ambapo aliwaomba waumini wote kuwa na upendo na kushirikiana katika kuifanya kazi ya Mungu.
Kwilemba amesema kanisa likiwa na upendo Mungu nae anakuwa na upendo mkubwa na kanisa lake kwa sababu Mungu anamuwazia mazuri kila mmoja hivyo na waumini kwa waumini wanatakiwa kuwaziana mazuri kila wakati.
"Yeremia 29: 11. siku za mwisho Mungu anaziwazia mema hata kama umelala vibaya ni juu yako kugundua Mungu anakuwazia nini yeye anakuwazia mazuri siku za mwisho pia Yeremia 1:4-5 inasema neno la bwana lilinijia, kusema,
kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa."amesema Kwilemba.
Kwa upande wake mchungaji kiongozi wa kanisa la JCC Charles Kwilemba akisoma historia ya kanisa hilo amesema kanisa lilianzishwa Agost 14,2022 likiwa na watumishi watano ambalo limesajiliwa kwa kuendesha shughuli zake za kiroho na za kimwili na makao makuu ni Temeke jijini Dar es salaam.
Akizungumzia mafanikio amesema kanisa lake lilianza na waumini watano, ndani ya mwaka mmoja limefanikiwa kuongeza waumini wasiopungua 45 na kanisa linaendelea kujengwa na lina eneo la hekari mbili na nusu.
"Maono yetu ni kujenga hospitali nzuri kwa ajili ya jamii,kujenga kanisa kubwa la kudumu lenye ghorofa moja na kuwafikia watu kwa njia mbalimbali ili waokoke na kuishi maisha ya kumpendeza Mungu."amesema Kwilemba.
"Pia tunampango wa kuanzisha darasa la awali na msingi ili watoto wapate sehemu nzuri ya kupatia elimu, pia kanisa linamshukuru mungu kwa kufikia hatua hii na tunawashukuri watu wote waliofika kwa ajili ya kumshukuru Mungu mahali hapa"amesema Kwilemba.
Mchungaji Kwilemba amesema Mungu amewasaidia wakajenga jengo la kanisa la muda na sasa wameanza kuweka ramani ya jengo lao la kudumu ambalo litakuwa ni jengo la ghorofa moja kwa ajili ya kumtukuza Mungu na wanategemea kujenga hospitali ya ghorofa moja ambayo itahudumia watu mbalimbali wakubwa na wadogo.
Askofu wa kanisa la Pefa lililopo Zanziba Daniel Kwilemba akihubiri neno la Mungu
Askofu wa kanisa la Pefa lililopo Zanziba Daniel Kwilemba akihubiri neno la Mungu
Mchungaji wa kanisa la JCC lililoko viwanja vya Mwadui kata ya Ngokolo
Mchungaji wa kanisa la JCC lililoko viwanja vya Mwadui kata ya Ngokolo akiwa na mama yake mzazi aloyevaa gauni la bluu
Mama yake na mchungaji Kwilemba akisalimia kanisa
Mama yake na mchungaji Kwilemba akisalimia kanisa
Mchungaji wa kanisa la JCC lililoko viwanja vya Mwadui kata ya Ngokolo akimtambulisha kwa waumini baba yake mkubwa
Mchungaji Charles Kwilemba akiwa na wazazi wake akimsifu Mungu
Waumini wa kanisa hilo wakimsifu Mungu
Waumini wa kanisa hilo wakimsifu Mungu
Waumini wa kanisa hilo wakimsifu Mungu
Wakisikiliza neno la Mungu
Waumini wakisikiliza neno la Mungu
Waumini wakisikiliza neno la Mungu
Waumini wakiomba
Mchungaji Charles akifafanua jambo
Mchungaji Charles akimlisha keki mama yake mzazi
Mchungaji Charles akiwalisha keki waumini ambayo iliandaliwa kanisani hapo
Mchungaji Charles akisalimiana na wageni waliohudhulia katika sherehe