BAADHI YA WANANCHI WAMEANZA KUELEWA CHANZO CHA MATUKIO MABAYA KWENYE JAMII






Baadhi ya wananchi wakitaka programu hiyo ifike ngazi za vijiji na vitongoji

Na Kareny Masasy,Shinyanga

BAADHI  ya wananchi mkoani Shinyanga  wameeleza kuelewa  changamoto  zinazotokea kwenye jamii za mtu mmoja mmoja kukosa maadili,wizi na kutojituma kwenye kazi  zinatoka na namna alivyolelewa  tangu kutungwa kwa mimba.

Yuster James  na Hamza Kusekwa wamesema hayo baada ya kusikiliza elimu ya sayansi ya makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto iliyotolewa na mtaalamu Andrew  Nkunga  kutoka mtandao wa Malezi na Makuzi nchini (TECDEN).

Kusekwa amesema mtoto anatakiwa  afundishwe tangu mimba inavyotungwa  suala hili linapendeza  lianze kufundishwa  kwenye mikutano ya vijiji au vitongoji ili wananchi wapate kuelewa.

“Mimi mwenyewe nilikuwa sijui  kama mama akiwa mjamzito mtoto tumboni anasikia kwenye hii ni sayansi  ingekuwa hivyo basi hata vitendo vya mauaji,uhalifu visingekuwepo kumbe  vinatokea  wazazi chanzo  kikubwa ”amesema  Kusekwa.

Katibu wa shujaa wa maendeleo wa kupinga ukatili wa kijinsia (SMAUJATA)  mkoa wa Shinyanga  Daniel Kapaya amesema   ameelewa   vitendo vya ukatili vinaanzia wapi kumbe   mtoto akiwa bado tumboni   anasikia vitendo vinavyotokea viwe vizuri au vibaya   kupitia programu hii kwa kujifunza wataendelea kutoa elimu kwa wazazi au walezi.

Mratibu  kutoka kituo cha msaada wa sheria (paceshi) John Shija  amesema kumekuwa na  kesi nyingi za kutelekezwa watoto kutupwa na kukosa malezi ya wazazi ikiwa  jamii  nayo imesahau jukumu la malezi  na hao wanaopewa kulea  baadhi   hawana nia juu ya malezi  wanafuta pesa.

Mrakibu  mwandamizi wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga anayesimamia dawati la jinsia  Monica Venancy amesema programu  jumuishi  ya malezi na makuzi  ameielewa  namna ilivyo kumbe  kizazi hiki kilichokosa maadili kuna sababu.

“ Kupitia program hii kwetu   imekuwa ni msaada wazazi wangefuata utaratibu huo hata kulawitiana,kubakana na msongo wa mawazo  kwenye jamii usingekuwepo zaidi kama ilivyosasa”alisema Venance.

Andrew Nkunga akitoa elimu hiyo amesema  hatua za makuzi kwa mtoto  zinaanzia umri 0 hadi miaka nane ikiwa ni  kipindi ambacho mtoto ubongo  unaanza kukua kama atapata changamoto kwenye ukuaji hata ukuaji wake hautakuwa timilifu.

 Akitambulisha program ya PJT-MMMAM  kwa niaba ya  mkurugenzi wa  shirika la  Investing in children and Strengthing their society ( ICS ) Sabrina  Majikata    amesema shirika la watoto duniani  (Unicef ) na  shirika la afya duniani (WHO) lilitengeneza framu  ya nguzo tano   kuhakikisha wanawekeza katika umri wa miaka mitatu lakini  taifa  la Tanzania liliangalia hilo nakuona kuwekeza katika  umri wa mwaka 0 hadi nane.

Majikata amesema mtoto  akiwa bado mdogo  ubongo unahitaji kujijenga zaidi  na kunatakiwa kutiliwe mkazo katika nguzo tano  ambazo ni  lishe,afyabora,Malezi yenye mwitikio,ujifunzaji wa awali na ulinzi na usalama.

Ofisa Maendeleo ya jamii  mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale  amesema  taasisi zinazolea watoto  ndani ya mkoa zinapatiwa mafunzo sababu zimekuwa zikiishi na watoto  wenye umri  mdogo kwa kusaidia wazazi wao   ili  wakue katika misingi bora.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu akiongea kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme amesema  watoto wanatakiwa wakue katika utimilifu na kulelewa katika nguzo tano muhimu zilizotajwa.

“Tumeelezwa duniani  kuna watoto taribani Millioni 250 wenye umri  chini ya miaka  mitano  na  hapa Tanzania kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi  ya mwaka 2022  kuna watoto zaidi ya Millioni 16 sawa na asilimia 27 hivyo tunapaswa kuwalinda ili wafikie hali ya  ukuaji timilifu”alisema Mkude

























Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464