WEADO YATOA ELIMU YA KUPINGA VITENDO VYA NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI KWA WANANCHI WA MASENGWA
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
SHIRIKA la WEADO limetoa elimu kwa wananchi wa Kata ya Masengwa wilayani Shinyanga, juu ya kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya watoto wadogo zikiwamo ndoa na mimba za utotoni.
Elimu hiyo imetolewa leo Septemba 7,2023, kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Center ya Masengwa na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Viongozi wa dini, wazee maarufu na Mabaraza ya Watoto.
Wananchi wa Masengwa wakisiliza elimu ya kupinga ndoa na mimba za utotoni.
Mkurugenzi wa Shirika la WEADO Eliasenya Nnko, akitoa elimu kwa wananchi wa Masengwa, ameitaka jamii kila mmoja awajibike katika ulinzi wa mtoto dhidi ya vitendo vya ukatili ikiwamo kuzuia mimba na ndoa za utotoni.
Mkurugenzi wa Shirika la WEADO Eliasenya Nnko.
"WEADO tunaiomba jamii ivunje ukimya dhidi ya mimba na ndoa za utotoni, toeni taarifa dhidi ya vitendo hivyo tunataka Masengwa vitendo hivi vibaki kuwa historia kusiwepo tena na mimba wala ndoa za utotoni," amesema Nnko.
"Lengo la mradi wetu huu ambao unafadhiliwa na Foundation For Civil Society kusiwepo na mimba wala ndoa za utotoni kabisa ibaki kuwa historia,"ameongeza.
Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Taifa Rafael Joseph, amewaomba wazazi wasiwafanyie ukatili watoto wao,bali wawapatie haki zao ikiwamo elimu na kuacha kuwaozesha ndoa za utotoni.
Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Taifa Rafael Joseph.
Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Masengwa Joyce Richard, amewataka akina Mama kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa za watoto wao kutaka kuozeshwa na siyo kukaa kimya na kuharibu ndoto zao.
"Mama unajukumu la kumlinda mtoto wako asiozeshwe ndoa za utotoni, vunjeni ukimya toeni taarifa kwa viongozi, pia msipeleke watoto wenu kuogeshwa dawa za mvuto wa mapenzi acheni wasome na kutimiza ndoto zao," amesema Joyce.
Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Masengwa Joyce Richard.
Mtendaji wa Kata ya Masengwa Hussein Majaliwa, amesema katika kukabiliana na vitendo vya kuzuia ndoa za utotoni, wamejiwekea mikakati kwamba hakuna ndoa yoyote kufungwa bila ya kupata kibali kutoka Mamlaka ya Serikali za Mitaa lengo ni kudhibiti ndoa za utotoni.
Amesema mkakati mwingine ni kuendelea kutoa elimu kwa jamii,kupitia Mikutano ya hadhara na vikao mbalimbali kuelimisha jamii juu ya madhara ya mimba na ndoa za utotoni, huku akisisitiza jamii kuendelea kuwalinda watoto.
Mtendaji wa Kata ya Masengwa Hussein Majaliwa.
Mwakilishi wa Baraza la watoto Mkoa wa Shinyanga Noelina Busisi.
Mwakilishi Baraza la Watoto Shule ya Sekondari Masengwa Francis Maige akizungumza akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mwakilishi Baraza la watoto Shule ya Msingi Masengwa Mayenga Mabula akizungumza kwenye Mkutano huo.
Afisa Elimu Kata ya Masengwa Juma Chiyamba akizungumza kwenye Mkutano huo.
John Eddy kutoka Shirika la WEADO akizungumza kwenye Mkutano huo.
Katibu wa Jukwaa la Wanawake Masengwa Hoka Jitulu akizungumza kwenye Mkutano huo.
Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Masengwa Joyce Richard akizungumza kwenye Mkutano huo.
Sheikh Soud Salamba akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mchungaji wa Kanisa la PAG Edward Salama akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mzee Maarufu Kata ya Masengwa Juma Ngelela akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mkutano wa kutoa elimu ya kupinga ndoa na mimba za utotoni kwa wananchi wa Masengwa ukiendelea.

Wananchi wa Masengwa wilayani Shinyanga wakiwa kwenye elimu ya kupinga ndoa na mimba za utotoni kutoka Shirika la WEADO.

Watoto wakisikiliza elimu ya kupinga vitendo vya ukatili zikiwamo ndoa na mimba za utotoni kwa kutakiwa kutoa taarifa dhidi ya vitendo ya ukatili.
Mkutano wa kutoa elimu ya kupinga ndoa na mimba za utotoni kwa wananchi wa Masengwa ukiendelea.
Mkutano wa kutoa elimu ya kupinga ndoa na mimba za utotoni kwa wananchi wa Masengwa ukiendelea.
Wananchi wa Masengwa wilayani Shinyanga wakiwa kwenye elimu ya kupinga ndoa na mimba za utotoni kutoka Shirika la WEADO.
Wananchi wa Masengwa wilayani Shinyanga wakiwa kwenye elimu ya kupinga ndoa na mimba za utotoni kutoka Shirika la WEADO.
Wananchi wa Masengwa wilayani Shinyanga wakiwa kwenye elimu ya kupinga ndoa na mimba za utotoni kutoka Shirika la WEADO.
Wananchi wa Masengwa wilayani Shinyanga wakiwa kwenye elimu ya kupinga ndoa na mimba za utotoni kutoka Shirika la WEADO.
Burudani zikitolewa kwenye utolewaji wa elimu ya kupinga mimba na ndoa za utotoni kwa wananchi wa Masengwa wilayani Shinyanga kutoka Shirika la WEADO.
Picha ya Pamoja ikipigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464