MKULIMA WA TUMBAKU ADAIWA KUJIPIGA RISASI AKIWA SHAMBANI KAHAMA


 MKULIMA MAARUFU WA TUMBAKU SAFARI MANJALA AMEDAIWA KUJIA  KWA KUJIPIGA RISASI KAHAMA
Mkulima maarufu wa Tumbaku Safari Manjala amedaiwa kujiua kwa kujipiga risasi akitumia bunduki yake aina ya Bastola akiwa kwenye shamba la miti yake katika kijiji cha Ilomelo kata ya Ulowa halmashauri ya Ushetu wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga.

Na Kadama Malunde.

Inaelezwa kuwa tukio hilo limetokea leo Ijumaa Septemba 8, 2023 majira ya saa mbili asubuhi ambapo Safari Manjala mkazi wa Kitongoji Namba Tisa A kijiji cha Ilomelo kata ya Ulowa anadaiwa kujipiga risasi mbili kidevuni na risasi kutokea kichwani.


Habari kutoka eneo la tukio zinasema Safari Manjala ameamka akiwa mzima na baada ya hapo alielekea kwenye msitu wake kisha akajipiga risasi.


Diwani wa Kata ya Ulowa Mhe. Gabriella Alphonce Kimaro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiwaomba wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi pindi wanapokuwa na msongo wa mawazo na badala yake watafute ushauri kwa watu wa karibu au viongozi.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limesema limepokea taarifa za tukio hilo na kwamba askari polisi tayari wamefika katika eneo la tukio.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464