RC MNDEME ATAKA KASI UJENZI SOKO KUU SHINYANGA
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, ameagiza kasi iongezwe ya ujenzi wa Miundombinu ya Soko Kuu la Manispaa ya Shinyanga, na kutoa mwezi mmoja likamilike, huku akiagiza pia katika ujenzi huo kitengwe chumba maalumu cha kunyonyeshea watoto.
Mndeme amebainisha hayo leo Septemba 11, 2023 alipotembelea kuona Maendeleo ya ujenzi wa ukarabati wa Miundombinu ya Soko hilo na kueleza kutoridhishwa na kasi yake ya ujenzi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akikagua ujenzi wa Soko Kuu Shinyanga.
Amesema kasi ya ujenzi wa Miundombinu ya Soko hilo hajaridhishwa nao, ambao ulipaswa kukamilika Aprili mwaka huu, na kuagiza hadi kufikia Oktoba 11 ujenzi wa vibanda vya chini uwe umekamilika, na vibanda vya juu vya ghorofa vikamilike Decemba 12 ili biashara zianze.
“Mimi siwezi kuwapakamafuta msema ukweli ni mpenzi wa Mungu, sijaridhishwa na kasi ya ujenzi wa miundombinu ya soko hili mpo nyuma, natoa mwezi mmoja vibanda vya chini viwe vimekamilika na kuanza biashara,”amesema Mndeme.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akikagua ujenzi wa Soko Kuu Shinyanga.
Aidha, amewataka wafanyabiashara kwamba katika upewaji wa vyumba hivyo vipya katika soko hilo, wasitumie Madalali wala kutoa Rushwa pamoja na kufanyabiashara halali, huku akitoa maagizo kasi iongezwe ya ukusanyaji mapato na kukamilisha miradi.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa ameagiza katika ujenzi wa Soko hilo na Masoko yote mkoani humo, likiwamo na Soko la Ndala, wahakikishe kuna kuwapo na chumba maalumu kwa ajili ya kunyonyeshea watoto na kucheza.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akikagua ujenzi wa Soko Kuu Shinyanga.
Naye Afisa Mipango wa Manispaa ya Shinyanga Michael Makotwe akisoma taarifa ya ujenzi wa ukarabati wa Soko hilo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, amesema ujenzi kwa sasa umefika asilimia 57.
Amesema ujenzi una husisha vyumba 106, ambapo vyumba 41 vya chini vipo katika hatua ya mwisho ya ukamilishaji na 65 bado vinaendelea na hatua ya ujenzi, na ujenzi huo hadi kukamilika kwake utagharimu Sh.bilioni 1.8 kwa kutumia fedha za mapato ya ndani.
Muonekano wa ujenzi wa Soko Kuu.
Kwa upande wake Fundi Mkuu wa ujenzi wa Soko hilo Deus Masalu amesema wameshindwa kukamilisha ujenzi huo kutokana na kukosekana kwa malighafi zikiwamo Kokoto na Saruji.
Nao baadhi ya wafanyabiashara wa Soko hilo akiwamo Issa Mwinamila, wameishukuru Serikali kwa kuwakarabatia miundombinu imara ya Soko hilo, ambapo watafanya biashara katika Mazingira Rafiki.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza na Wafanyabiashara wa Soko Kuu Manispaa ya Shinyanga, alipotembea kuona Maendeleo ya ukarabati wa Miundombinu ya Soko hilo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza kwenye Mkutano wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu Manispaa ya Shinyanga.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye Mkutano wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu Manispaa ya Shinyanga.
Afisa Mipango Manispaa ya Shinyanga Michael Makotwe akisoma taarifa ya ukarabati wa ujenzi wa Soko Kuu Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze akizungumza kwenye Mkutano wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti TCCIA Mkoa wa Shinyanga Jonathan Manyama,akizungumza kwenye Mkutano wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu Manispaa ya Shinyanga.
Fundi Mkuu wa ujenzi wa Soko Kuu la Manispaa ya Shinyanga Deus Masala akielezea Changamoto za kukwamisha ujenzi wa Soko hilo kukamilika kwa wakati.
Mfanyabiashara wa Soko Kuu Manispaa ya Shinyanga Issa Mwinamila akitoa shukrani kwa Serikali juu ya ukarabati wa Miundombinu ya Soko hilo.
Mfanyabiashara Gerald Mkenda akizungumza kwenye Mkutano wa Mkuu wa Mkoa na Wafanyabiashara wa Soko Kuu Manispaa ya Shinyanga.
Mfanyabiashara Sarah Michael akizungumza kwenye Mkutano wa Mkuu wa Mkoa na Wafanyabiashara wa Soko Kuu Manispaa ya Shinyanga.
Mfanyabiashara Manka Vicent akizungumza kwenye Mkutano wa Mkuu wa Mkoa na Wafanyabiashara wa Soko Kuu Manispaa ya Shinyanga.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme na Wafanyabiashara wa Soko Kuu Manispaa ya Shinyanga.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme na Wafanyabiashara wa Soko Kuu Manispaa ya Shinyanga.
Mkutano wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu Manispaa ya Shinyanga na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme ukiendelea.

Muonekano wa ukarabati wa ujenzi wa miundombinu ya Soko Kuu Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kushoto)akiwa na Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko wakishiriki ujenzi wa Soko Kuu Manispaa ya Shinyanga ili ukamilike kwa wakati.
Muonekano wa ujenzi wa ukarabati Miundobinu ya Soko Kuu Manispaa ya Shinyanga.

Mafundi wakiendelea na ujenzi.
Mafundi wakiendelea na ujenzi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiwa katika ujenzi wa ukarabati wa miundombinu ya Soko Kuu Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akisalimia na baadhi ya Wafanyabiashara wa Soko Kuu Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akipiga picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyabiashara wa Soko Kuu Manispaa ya Shinyanga.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464