TAASISI YA TAWEN YATAMBULISHWA MWANZA

TAASISI YA TAWEN YATAMBULISHWA MWANZA

TAASISI ya Tanzania Women Empowerment Network (TAWEN) ambayo inajihusisha na uwezeshaji wanawake na vijana kiuchumi hapa nchini Tanzania, imetambulishwa rasmi Jijini Mwanza.

Utambulisho huo umefanyika Septemba 2, 2023 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, na kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo Daniel Machunda.
Mwenyekiti wa Taasisi ya TAWEN Kanda ya Ziwa Neema Edward Mgobela ambaye pi ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Ukerewe, amesema hivi karibuni wanatarajia kuanzisha Tawi la Taasisi hiyo Jijini Mwanza, ndiyo maana wameanza kwanza kuitambulisha kwa viongozi ili waifahamu.

“Taasisi yetu ya TAWEN inajihusisha na uwezeshaji wanawake na vijana kiuchumi, na hapa Jijini Mwanza tunatarajia hivi karibuni kuanzisha Tawi na tutafanya uzinduzi,”amesema Neema.
Aidha, Kaimu Katibu Tawala huyo ameipongeza Taasisi hiyo pamoja na kuikaribisha Jijini Mwanza kufanyakazi ya kuinua kiuchumi vijana na wanawake.
Mwenyekiti wa Taasisi ya TAWEN Kanda ya Ziwa Neema Edward Mgobela (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Daniel Machunda (kulia) na Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Mipango Mkoa wa Mwanza Emil Kasagara
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464