RC MNDEME ATANGAZA NEEMA KWA WAKULIMA WA ZAO LA PAMBA,TUMBAKU
Na Marco Maduhu, KAHAMA
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amewahakikishia Wakulima wa zao la Pamba, Tumbaku na mazao mengine, kwamba Serikali chini ya Rais Samia itaendelea kusimamia maslahi ya Mkulima pamoja kuwapatia Pembe Jeo na kuongeza uzalishaji ambao utawainua kiuchumi.
Amebainisha hayo leo Septemba 17,2023 alipofanya ziara kwenye Kiwanda cha kuchakata zao la Pamba (Ginnery) katika Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU)pamoja na kuzungumza na Wakulima wa Pamba,Tumbaku na wafanyakazi wa Kiwanda hicho.
Amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia ipo bega kwa bega na Wakulima kwa kuhakikisha ina wawekea mazingira mazuri ya Kilimo kwa kuwapatia Pembe Jeo, bei nzuri pamoja na kulinda Maslahi yao, ikiwamo kulipwa pesa zao kwa wakati za mauzo ya mazao yao.
"Katika Mwaka wa fedha (2022/2023) Serikali chini ya Rais Samia katika Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) imetoa kiasi cha Sh.bilioni 148 kwa ajili ya Mbegu za Pamba, Viuavidudu, na Vinyunyizi na kuonyesha kiasi gani inavyo mjali Mkulima,"amesema Mndeme.
Aidha, amesema Serikali pia itawamegea eneo ulipokuwa Mgodi wa dhahabu Buzwagi Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU)ili kianzishe Kiwanda cha kutengeneza nguo na kuongeza thamani ya zao la Pamba, huku akiwasisitiza pia mwakani waanzishe na Kiwanda cha Mafuta ya Pamba na chakula cha mifugo.
Ametoa wito pia kwa Wakulima wa Pamba waache pia tabia ya kuchafua zao hilo kwa kuchanganya Udongo, Machanga na Mawe, ili Pamba ya Tanzania iendelee kuwa na ubora na nyeupe na kuongezeka thamani na hata bei kuwa juu.
Akizungumzia zao la Tumbaku, amesema bei ya Tumbaku imeongezeka kutoka Dola 1.6 hadi Dola 2.huku akitoa agizo kwamba Wakulima wa Tumbaku ambao bado hawajalipwa fedha zao za mauzo ya zao hilo walipwe haraka.
" Kuna Kampuni Mbili ya Mkwawa na Voedsel kushindwa kumlipa Mkulima wa Tumbaku fedha zake kwa wakati, ambazo nizaidi ya Bilioni 20, hivyo naagiza Mkuu wa wilaya hadi Ijumaa Ijayo nipewe taarifa Wakulima hawa wawe wameshalipwa fedha zao, vinginevyo wachukuliwe hatua na kuzuiwa kabisa kununua Tumbaku," amesema Mndeme.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akitupia Pamba katika Cherehani ya uchambuzi wa Pamba na Mbegu.
Amesema kwa upande wa vyama 12 vya Msingi vya Ushirika (AMCOS), ambavyo vimeshindwa kurejeshea marejesho ya Mkopo Benki, na kuzitia hasara Benki na Mkulima watafutwe, pamoja na Takukuru kufanya uchunguzi na watakao bainika Wachukuliwe wachukuliwe hatua.
Mndeme amemuagiza pia Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoani Shinyanga Hilda Boniphace,kufanya Marekebisho ya Mkataba wa Mkopo,kwamba Kampuni za ununuaji mazao wakichelewa kulipa madeni benki asitozwe riba Mkulima bali Kampuni sababu Mkulima yeye ameshauza mazao yake.
Ameagiza pia vyama vya Msingi ya Ushirika 12 ambavyo vimekufa vifufuliwe, na hakuna kuanzisha vyama vingine.
Naye Meneja KACU Abduli Ally, akisoma taarifa ya Chama hicho kwa Mkuu wa Mkoa, amesema wanaipongeza Serikali kwa kumjali Mkulima na kuwa wekea mazingira mazuri ya Kilimo, na hata kukifufua chama hicho baada ya kusimama tangu mwaka 2013 na kufufuliwa 2020.
Meneja KACU Abduli Ally.
Amesema KACU imesajiliwa Mwaka 1994 ina wanachama 126, ambapo 36 wanajishughulisha na zao la Pamba, wanachama 46 zao la Tumbaku, na 44 mazao yote mawili.
Ametaja Changamoto ambazo zinawakabili kuwa ni vyama 12 vya Msingi kushindwa kurejesha madeni ya mikopo ya pembe jeo kwenye mabenki kwa asilimia 100, na kushindwa kulipa wakulima.
Pia baadhi ya Kampuni za ununuzi wa Tumbaku zikiwano Mkwawa na Voedesl kuchelewa kulipa malipo ya mauzo ya Tumbaku kwa baadhi ya Wakulima kwenye AMCOS, pamoja na kukatika kwa umeme mara kwa mara na kuathiri uzalishaji wa Pamba Nyuzi na Mbegu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiangalia Mbegu za Pamba.
Ametaja mipango waliyonayo KACU kwamba ni kuongeza thamani ya Mbegu wanayozalisha kwa kuanzisha Kiwanda cha kukamua mafuta yatokanayo na Mbegu za Pamba ujenzi ambao utaanza mwakani.
Naoa baadhi ya Wakulima wa Tumbaku wamemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kutoa maelekezo juu ya kulipwa pesa zao za mauzo ya zao hilo,ambapo walikuwa hawajui hatima yao ya kulipwa fedha hizo, huku wakiipongeza Serikali kwa kumjali Mkulima.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza na Wakulima wa Pamba, Tumbaku, Wafanyakazi wa Kiwanda cha kuchakata zao la Pamba na viongozi mbalimbali wa Serikali na AMCOS katika Ginnery ya KACU.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita akizungumza katika ziara hiyo ya KACU.
Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoani Shinyanga Hilda Boniphace akizungumza katika ziara hiyo ya KACU.
Mbunge wa Ushetu Emmanuel Cherehani akizungumza katika ziara hiyo ya RC Mndeme, KACU.
Mwenyekiti wa KACU Tano Nsabi akizungumza katika ziara hiyo ya RC Mndeme.
Mkulima Maria Shija akitoa shukrani kwa Serikali kujali Wakulima na kupigania maslahi yao.
Wafanyazi wa Kiwanda cha Pamba KACU, Wakulima wa Pamba na Tumbaku na viongozi mbalimbali wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa.
Mkutano wa Mkuu wa Mkoa ukiendelea.
Mkutano wa Mkuu wa Mkoa ukiendelea.
Wafanyazi wa Kiwanda cha Pamba KACU, Wakulima wa Pamba na Tumbaku na viongozi mbalimbali wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa.
Mkutano wa Mkuu wa Mkoa ukiendelea.
Wafanyazi wa Kiwanda cha Pamba KACU, Wakulima wa Pamba na Tumbaku na viongozi mbalimbali wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa.
Mkutano wa Mkuu wa Mkoa ukiendelea.
Mkutano wa Mkuu wa Mkoa ukiendelea.
Wafanyazi wa Kiwanda cha Pamba KACU, Wakulima wa Pamba na Tumbaku na viongozi mbalimbali wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Sginyanga Christina Mndeme akiangalia mashine ya kusafisha Pamba.
Mkuu wa Mkoa wa Shunyanga Christina Mndeme akiangalia ubora za Pamba.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiendelea na ziara katika Kiwanda cha kuchakata zao la Pamba KACU.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiendelea na ziara katika Kiwanda cha kuchakata zao la Pamba KACU.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiendelea na ziara katika Kiwanda cha kuchakata zao la Pamba KACU.
Picha ya pamoja ikipigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464