UJENZI WA SHULE MPYA YA SEKONDARI KUWAONDOLEA ADHA WANAFUNZI KUSOMA SHULE UMBALI MREFU
Na Marco Maduhu, KAHAMA
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, ameweka Jiwe la Msingi katika ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Ngilimba iliyopo Kata ya Ulowa Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama, ambayo itawaondolea adha wanafunzi kutembea umbari mrefu kwenda shule.
Ameweka jiwe hilo la Msingi leo Septemba 18,2023, na kuwataka wazazi wapeleke shule watoto wao ili wasome na kutimiza ndoto zao.
Amesema Rais Samia ametoa kiasi cha fedha Sh.milioni 603.8 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo mpya ya Sekondari Ngilimba Kata ya Ulowa,ili kuondoa adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu, bali wasome shule wakiwa karibu na kufanya vizuri kitaaluma na kutimiza ndoto zao.
"Shukrani ambayo mtampatia Rais katika ujenzi wa shule hii mpya ya Sekondari Ngilimba,ni kupeleka watoto wenu kwa wingi kusoma,pamoja na kumuombea Rais afya njema ili aendelee kutafuta pesa na kuwaletea maendeleo," amesema Mndeme.
Aidha, ameiagiza Halmashauri ya Ushetu kutenga fedha za mapato ya ndani, kwa ajili ya kujenga mabweni katika shule hiyo mpya,ili wanafunzi wabaki hapo shuleni wakijisomea na kufanya vizuri katika masomo yao.
Katika hatua nyingine Mndeme, amepongeza kasi ya ujenzi wa shule hiyo, huku akiagiza pia ujenzi wake ujengwe kwa kiwango bora.
Amempongeza pia Mwananchi Magazi Andrew ambaye ametoa eneo kujengwa shule hiyo, lenye ukubwa wa hekali 12 kwa kuonyesha uzalendo ambapo amempatia zawadi ya mbuzi.
Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ulowa Godfrey Msimbe, amesema ujenzi wa shule hiyo mpya licha ya kuondoa msongamano wa wanafunzi katika shule mama, pia itaondoa kero ya wanafunzi kutembea umbali mrefu zaidi ya Kilomita 10 hadi 17,na ujenzi wake upo hatua nzuri.
Nao baadhi ya wazazi akiwamo Anjela Shigemo,wamepongeza ujenzi wa shule hiyo ya Sekondari Ngilimba,ambayo itaondoa tatizo la watoto wao kutembea umbali mrefu kwenda shule, na wengine wamekuwa wakishindwa kwenda shule kutokana na kuchoka sababu ya umbali.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ngilimba Kata ya Ulowa Halmashauri ya Ushetu wilyani Kahama.
Mkuu wa Sekondari ya Ulowa Godfrey Msimbe akisoma taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme juu ya ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari ya Ngilimba.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme wapili kutoka (kulia) akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Ngilimba iliyopo Kata ya Ulowa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akishiriki ujenzi katika shule hiyo mpya ya Sekondari Ngilimba iliyopo Kata ya Ulowa Halmashauri ya Ushetu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akishiriki ujenzi katika shule hiyo mpya ya Sekondari Ngilimba iliyopo Kata ya Ulowa Halamshauri ya Ushetu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akishiriki ujenzi katika shule hiyo mpya ya Sekondari Ngilimba iliyopo Kata ya Ulowa Halmashauri ya Ushetu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akishiriki utengenezaji wa Mlango katika shule hiyo mpya ya Sekondari Ngilimba iliyopo Kata ya Ulowa Halmashauri ya Ushetu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akikagua ujenzi wa Maabara za Sayansi katika Shule hiyo Mpya ya Sekondari Ngilimba.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akikagua ujenzi wa Maabara za Sayansi katika Shule hiyo Mpya ya Sekondari Ngilimba.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiweka Jiwe la Msingi katika ujenzi wa Shule hiyo mpya ya Sekondari Ngilimba Kata ya Ulowa Halmashauri ya Ushetu.
Muonekano wa Jengo la Utawala.
Baadhi ya vyumba vya Madarasa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme wapili kutoka (kulia) akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Ngilimba iliyopo Kata ya Ulowa Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464