RC MNDEME ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI SESEKO NA KUZITATUA
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amesikiliza kero za wananchi wa Kijiji cha Seseko Kata ya Mwamalili Manispaa ya Shinyanga na kuzitatua.
Amefanya Mkutano huo jana katika Kijiji hicho cha Seseko,ambapo wananchi waliwasilisha kero zao mbalimbali ikiwamo ukosefu wa huduma ya umeme, maji kukatikati mara kwa mara, na mlipuko wa Magonjwa ya Ng'ombe.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (katikati)akisikiliza kero za wananchi.
Mndeme akijibu kero hizo, amezitaka Mamlaka husika ambazo zimeguswa na malalamiko hayo ya wananchi kuyafanyia kazi na kutoa huduma stahiki kwao.
Aidha,amesema Serikali chini ya Rais Samia katika Mkoa huo wa Shinyanga ametoa kiasi cha fedha Sh.Trilioni Moja kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi na kuwahidi wananchi kwamba kero zote ambazo zinawakabili zitatuliwa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kushoto)akiwa na Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko.
"Wananchi kero zenu zote ambazo mmeziwasilisha hapa zitashughulikiwa,"amesema Mndeme.
Aidha, amewataka wananchi kuendelea kumuunga Mkono Rais Samia katika utawala wake ili aendelee kuwaletea maendeleo.
Baadhi ya wananchi wa Seseko, waliomba kero zao ambazo wameziwasilisha zifanyiwe kazi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara na wananchi wa Seseko.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza kwenye Mkutano huo wa hadhara.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye Mkutano huo.
Wananchi wa Seseko wakiwa kwenye Mkutano wa Mkuu wa Mkoa.
Mwananchi akiwasilisha kero.
Wananchi wa Seseko wakiwa kwenye Mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Wananchi wa Seseko wakiwa kwenye Mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Wananchi wa Seseko wakiwa kwenye Mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Wananchi wa Seseko wakiwa kwenye Mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464