MAHAFALI YA KWANZA DARASA LA 7 SHULE YA MSINGI IHELELE ILIYO ASISIWA NA KASHWASA YAFANA
Na Marco Maduhu,IHELELE
SHULE ya Msingi Ihelele iliyopo wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, ambayo ilianzishwa kwa wazo la aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga (KASHWASA) Mhandisi Clement Kivegalo, imefanya Mahafali ya kwanza ya darasa la Saba.
Mahafali hayo yamefanyika leo Septemba 29,2023 katika shule hiyo huku Mgeni Rasmi akiwa ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi KASHWASA Dk.Edith Kwezi akimwakilisha Mwenyekiti wa Bodi hiyo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ihelele Evidence Muganyizi,akisoma taarifa ya shule hiyo, amesema ilianza kujengwa mwaka 2014 na kuanza kutoa elimu mwaka 2017 ikiwa na jumla ya wanafunzi 94, wavulana 40, Wasichana 54.
"Wazo la ujenzi wa shule hii ya Msingi Ihelele lilitoka kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa KASHWASA Mhandisi Clement Kivegalo,ndipo jamii ikahamasika na kuchangia nguvu kazi na kufanikisha ujenzi wa shule, na leo watoto wanahitimu elimu ya darasa la 7,"amesema Muganyizi.
Amesema KASHWASA imeendelea kuwa na Mchango mkubwa kwenye Shule hiyo, kwa kuchangia ujenzi wa miundombinu mbalimbali na utoaji wa Madawati.
Aidha, ametaja idadi ya wanafunzi ambao wamehitimu darasa la Saba kuwa 71, Wasichana 42 na Wavulana 29.
Katika hatua nyingine ametaja changamoto ambazo bado zinawakabili shuleni hapo kuwa ni upungufu wa nyumba za walimu, ukosefu wa maji, umeme, uwanja wa michezo na vifaa vya michezo.
Pia,ameishukuru KASHWASA kwa kuwajengea nyumba moja ya Mwalimu ambayo anaishi yeye pamoja na kuwaunga Mkono kutoa Sh.milioni 1 kuanzisha ujenzi wa nyumba nyingine ya Walimu, huku Kamati ya Shule ikichangia mifuko 5 ya Saruji.
Naye Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya KASHWASA Dk. Edith Kwezi akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo, amesema Changamoto zote ambazo zimewasilishwa watazifanyia kazi,huku akiwasihi wazazi kuwasomesha watoto wao na kuhakikisha wanahitimu elimu zao na siyo kuishia njiani.
Amesema katika shule hiyo wanafunzi walioanza kusoma darasa la kwanza walikuwa 94 lakini leo wanahitimu 71 na kuwataka wazazi wasiruhusu watoto wao kuishia njiani ili wasome na kutimiza ndoto zao.
Ametoa wito pia kwa wanafunzi ambao wamehitimu darasa la 7,kwamba bado wanasafari ndefu katika kujenga mstakabali wa maisha yao na kuwa wale watakao faulu kujiuga na kidato cha kwanza waendelee kusoma kwa bidii hadi wafike Chuo Kikuu na kutimiza ndoto zao na hata kuja kuwa viongozi wa taifa hili.
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi KASHWASA Dk.Edith Kwezi akizungumza kwenye Mahafali hayo.
Meza Kuu wakiwa kwenye Mahafali hayo.
Wahatimu wa darasa la Saba katika Shule ya Msingi Ihelele wakiwa kwenye Mahafali yao.

Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya KASHWASA DK.Edith Kwezi akitoa vyeti kwa wahitimu wa darasa la Saba Shule ya Msingi Ihelele.
Zoezi la utoaji vyeti likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti likiendelea.
Wahitimu darasa la Saba wakitoa burudani.
Wahitimu darasa la Saba wakiendelea kuimba nyimbo kwenye Mahafali yao.
Wahitimu darasa la Saba Shule ya Msingi Ihelele wakiendelea kutoa burudani.
Wahitimu darasa la Saba Shule ya Msingi Ihelele akiimba nyimbo za kuwaaga wanafunzi wenzao.
Wahitimu darasa la Saba Shule ya Msingi Ihelele akiimba nyimbo za kuwaaga wanafunzi wenzao.
Wazazi wakiwa kwenye Mahafali ya watoto wao ambao wamehitimu elimu ya darasa la Saba shule ya Msingi Ihelele.
Mahafali ya darasa la Saba Shule ya Msingi Ihelele yakiendelea.

Awali Mgeni Rasmi akiwasili kwenye Mahafali ya darasa la Saba Shule ya Msingi Ihelele.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464