KLABU YA WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA IMEENDESHA MDAHALO TATIZO LA KUKATIKA UMEME


KLABU YA WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA IMEENDESHA MDAHALO TATIZO LA KUKATIKA UMEME

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

KLABU ya Waandishi wa Habari Mkoani Shinyanga imeendesha Mdahalo wa wadau kwa ajili ya kujadili na kutoa maoni juu ya Suluhisho la kukatika kwa umeme hapa nchini.

Mdahalo huo umefanyika leo Septemba 30, 2023 na kushirikisha wadau kutoka Sekta mbalimbali wakiwamo Wafanyabiashara, Wajasiriamali, Asasi za Kiraia,Wananchi, Taasisi za Umma, Dini, Vyama vya Siasa na TANESCO.
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Shinyanga Patrick Mabula akizungumza kwenye Mdahalo huo, amesema wameundesha kwa ajili ya wadau kutoa maoni yao ili kumaliza tatizo la kukatika kwa umeme hapa nchini kwa maslahi mapana ya uchumi wanchi.

Amesema mdahalo huo ni sehemu ya wananchi kutoa mawazo yao chanya, yatakayo weza kuleta mabadiliko kwa Mamlaka husika za Serikali zinazohusiana na Nishati ya Umeme na kuchukua hatua,ili tatizo la kukatika kwa umeme lipate kukoma hapa nchini na wananchi waendelee na shughuli zao za uzalishaji kupitia umeme na kukua kiuchumi.

“Mdahalo huu wa Nishati ya Umeme ni Tija ya Uchumi wa Ustawi wa Maendeleo hapa nchini, kupitia maoni ya wadau ambayo watayatoa hapa, Mamlaka husika watachukua mawazo haya na kuyafanyia kazi, ili kumaliza kabisa tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara,”amesema Mabula.
Nao Wadau wakichangia Mada kwenye Mdahalo huo, wamesema ili kumaliza tatizo la kukatika kwa umeme kwamba Serikali inapaswa iache kutumia chanzo kimoja cha uzalishaji Umeme cha Maji, bali watumie vyanzo vingine ikiwamo Gesi,Upepo, Joto la Ardhi na Umeme wa Jua.

Wamesema kuendelea kutumia Chanzo cha Maji pekee kuzalisha Umeme likiwamo Bwawa la Mwalimu Nyerere ambalo ndilo linategemewa kumaliza tatizo la kukatika kwa umeme hapa nchi, kwamba tatizo hilo haliwezi kukoma bali litaendelea kuwa vile vile, na kwamba Serikali inapaswa itumie vyanzo vingine kuzalisha umeme na siyo maji tu.
Aidha,wadau hao wamesema tatizo la kukatika kwa umeme limekuwa likiathiri shughuli zao na hata kuwarudisha nyuma kiuchumi, na linatishia pia wawekezaji kuogopa kuja kuwekeza hapa nchini kutokana hakuna umeme wa uhakika.

Naye Dk, Meshack Kulwa, ametoa maoni kwa Serikali kuruhusu Makampuni binafsi kuwekeza kwenye Nishati ya Umeme ili kuwepo na ushindani kwa TANESCO, jambo ambalo tatizo la kukatika kwa umeme litabaki kuwa historia hapa nchini.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Elias Turnbull, ambaye ni Meneja wa TANESCO wilaya ya Kishapu, amesema tatizo la kukatika kwa umeme kwamba matumizi ya umeme yamekuwa makubwa lakini uzalishaji ni kidogo,kutokana na vyanzo vya uzalishaji umeme kutokuwa na maji mengi.
Amesema matumizi ya umeme kwa nchi nzima kwa sasa ni Megawatts 1,482.8 lakini uzalishaji upo chini ya Megawatts 1,000, na kwamba vyanzo vyote vya uzalishaji umeme vingekuwa vinafanya kazi umeme ungezalishwa Megawatts 1,570 na kusingekuwapo na kero ya kukatika kwa umeme mara kwa mara.

Amesema Serikali imeendelea kuchukua hatua ya kumaliza kwa tatizo la kukatika kwa umeme ikiwamo na ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere ambalo litakuwa likizalisha Meggawats 2,115 na litakamilika hivi karibuni na tatizo la kukatika kwa umeme nchini litabaki kuwa historia.
Aidha, amesema pia Serikali imeendelea kuibua vyanzo vingine vya uzalishaji umeme, ikiwamo umeme wa Jua ambao unatekelezwa wilayani Kishapu Megawatts 150, na kwamba katika Mkoa wa Shinyanga mradi huo ukikamilika hakutakuwa na tatizo la umeme sababu matumizi ya umeme kwa Mkoa huo ni Megawatts 70.

Rais Samia hivi karibuni alitoa miezi Sita kwa Mkurugenzi Mpya wa Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Gissima Nyamo Hanga kwamba ndani ya miezi sita asisikie tena tatizo la Mgao wa umeme.
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Shinyanga Patrick Mabula akizungumza kwenye Mdahalo huo.
Meneja wa TANESCO wilaya ya Kishapu Mhandisi Elias Tunrbull akizungumza kwa niaba ya Meneja TANESCO Mkoa wa Shinyanga kwenye Mdahalo huo.
Afisa Uhusiano huduma kwa wateja TANESCO Mkoa wa Shinyanga Emma Nyaki akizungumza kwenye Mdahalo huo.
Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara,Viwanda na Kilimo Mkoa wa Shinyanga TCCIA Jonathani Manyama akizungumza kwenye Mdahalo huo.
Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara,Viwanda na Kilimo Mkoa wa Shinyanga TCCIA Jonathani Manyama akizungumza kwenye Mdahalo huo.
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Ally Majeshi akizungumza kwenye Mdahalo huo.
Dk,Meshack Kulwa akichangia Mada kwenye Mdahalo huo.
Mdau wa umeme Crytus Kabete akichangia Mada kwenye Mdahalo huo.
Afisa wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga akichangia Mada kwenye Mdahalo huo.
Wadau wa umeme wakiwa kwenye Mdahalo.
Wadau wa umeme wakiwa kwenye Mdahalo.
Wadau wa umeme wakiwa kwenye Mdahalo.
Wadau wa umeme wakiwa kwenye Mdahalo.
Mdahalo ukiendelea.
Wadau wa umeme wakiendelea kuchangia Mada kwenye Mdahalo huo.
Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga Estormine Hennry akichangia Mada kwenye Mdahalo huo.
Wadau wakiendelea kuchangia Mada kwenye Mdahalo.
Mwandishi wa Habari Radio Kwizera Amos John akichangia Mada kwenye Mdahalo huo.
Wadau wa umeme wakiwa kwenye Mdahalo.
Mwandishi wa habari kutoka Jambo FM Yunis Kanumba akichangia Mada kwenye Mdahalo huo.
Wadau wa umeme wakiwa kwenye Mdahalo.
Wadau wa umeme wakiwa kwenye Mdahalo.
Mdau wa umeme Yusuph Hamis akichangia Mada kwenye Mdahalo huo.
Mdahalo ukiendelea.
Mwandishi wa habari wa Star tv Shabani Alley akichangia Mada kwenye Mdahalo huo.
Wadau wa umeme wakiwa kwenye Mdahalo.
Wadau wakiendelea kuchangia Mada kwenye Mdahalo huo.
Wadau wa umeme wakiwa kwenye Mdahalo.
Mdau wa umeme Chief Abdala Sube akichangia Mada kwenye Mdahalo huo.
Mwandishi wa Habari wa AZAM TV Kasisi Costa akisherehesha Mdahalo huo.
Mdahalo ukiendelea.
Wadau wa umeme wakiwa kwenye Mdahalo.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Miti Mirefu Nassoro Warioba akixchangia Mada kwenye Mdahalo huo.
Wadau wa umeme wakiwa kwenye Mdahalo.
Wadau wa umeme wakiwa kwenye Mdahalo.
Mdahalo ukiendelea.
Wadau wa umeme wakiwa kwenye Mdahalo.
Mdahalo ukiendelea.
Wadau wa umeme wakiwa kwenye Mdahalo.
Picha ya Pamoja ikipigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464