Header Ads Widget

UWT WATOA VYETI VYA PONGEZI KWA VIONGOZI SHINYANGA ZIARA YA MWENYEKITI WA UWT TAIFA MARY CHATANDA

UWT watoa vyeti vya pongezi kwa viongozi Shinyanga ziara ya Mwenyekiti UWT Taifa Mary Chatanda

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

UMOJA wa wanawake Tanzania Mkoa wa Shinyanga (UWT), umetoa vyeti vya pongezi kwa viongozi wa Mkoa huo kwa kusimamia na kufanikisha ziara ya Mwenyekiti wa (UWT) Taifa Mary Chatanda.

Vyeti hivyo vimetolewa jana na Katibu wa UWT Mkoa wa Shinyanga Asha Kitandala, akiwa na Mjumbe wa UWT Christina Gule, pamoja na Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Ukerewe Neema Magobela ambaye aliambatana kuwa unga mkono.
UWT wakimpatia Cheti cha Pongezi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme.

Akizungumza katika makabidhiano ya vyeti hivyo Katibu wa UWT Mkoa wa Shinyanga Asha Kitandala, amesema viongozi wa Mkoa huo wakiwamo Mkuu Mkoa ,Wakuu wa wilaya na vyombo vya Dola walifanya kazi kubwa katika kukakikisha ziara hiyo inakwenda vizuri na kuhitimishwa salama.

"Katika ziara hii viongozi mbalimbali walituunga Mkono akiwamo Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi kutoa Tripu 10 za mchanga kufanikisha ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UWT," amesema Kitandala.
UWT wakimpatia Cheti ya Pongezi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi.
UWT wakimpatia Cheti ya Pongezi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi.

"Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita yeye ametoa tofari 500 kufanikisha ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UWT tunawapongeza kwa kutuunga Mkono," ameongeza.
UWT wakimpatia cheti cha Pongezi Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita.

Aidha,ziara ya Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda aliifanya Mkoani Shinyanga kuanzia Agost 25 hadi 29 akiwa ameambatana na Makamu wake pamoja na Wajumbe wa NEC kukagua miradi ya maendeleo na kuimarisha Jumuiya ya UWT.
UWT wakimpatia cheti cha pongezi Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo.
UWT wakiwa katika picha ya pamoja.

Post a Comment

0 Comments