POLISI SHINYANGA WAKAMATA MASHINE YA KUFUA UMEME

POLISI SHINYANGA WAKAMATA MASHINE YA KUFUA UMEME

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

JESHI la Polisi mkoani Shinyanga limekamata vitu mbalimbali vya wizi ikiwamo mashine ya kufua umeme (Generator), silaha ambayo ilikuwa ikitumika katika uhalifu,madawa ya kulevya,noti bandia 15 zenye thamani ya Sh. 150,000 pamoja na lita 76 za Gongo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi amebainisha hay oleo Septemba 21, 2023 wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Agosti hadi Septemba.
Amesema kwa kipindi hicho wamefanikiwa kukamata vitu mbalimbali vya wizi pamoja na silaha aina ya Shortgun ambayo ilikuwa ikitumika katika matukio ya uhalifu, pamoja na silaha nyingine ambayo ilikuwa ikimilikiwa isivyo halali, pamoja na madawa ya kulevya aina ya Bangi Kilogram 40, Kete 18 na Heroine Kete Moja.

Ametaja vitu vya wizi ambavyo wamevikamata katika msako huo kuwa ni Sub-Woofer moja, Tv Moja, Viti 20, Mashine ya kufua umeme, kuchomelea vyuma. lita 120 za mafuta ya kuendeshea mitambo pamoja vipande 880 vya Nondo.
Mashine ya kufua umeme ambayo imeibiwa.

Aidha, amesema pia wamekamata waganga watatu wa kienyeji kwa kufanya shughuli za uganga na vifaa mbalimbali vya kupiga ramli chonganishi pamoja na Pikipiki 16 zilizokuwa zikitumika kutenda makosa mbalimbali.

“Katika Msako huu jumla ya watuhumiwa 12 tunawashikilia kuhusiana na makosa haya ya uhalifu, na wengine tumeshawafikisha tayari mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria na baadhi wamepewa dhamana wakisubili upelelezi kukamilika,”amesema Magomi.
Amesema katika mashauri ambayo yalikuwa yakiendelea Mahakamani, wamefanikiwa kufunga Jela maisha mtuhumiwa mmoja wa kesi ya ubakaji, na wengine 4 wa kesi ya ubakaji kuhukumiwa miaka 30, kesi za wizi 3 watuhumiwa walilipa faini, kutelekeza familia kufungwa miazi 6, kutorosha mwanafunzi viboko 6.

Ametaja Kesi nyingine zilizotolewa hukumu kuwa ya kutupa Mtoto miaka miwili jela, upatikanaji madawa ya kulevya kesi mbili watuhumiwa wamefungwa miaka miwili, na kesi ya kuoatikana na bangi mtuhumiwa alihukumiwa kuitumika jamii ndani ya mwezi mmoja.
Katika hatua nyingine ametaja makosa ya usalama Barabarani na walifanikiwa kukamata Magari 2,850 ambayo ni mabovu, 1,053 kuzidisha abiria, 163 kutokuwa na bima, kuendesha kwa njia hatarishi 139, kutofunga mkanda 31, bila lessen 5 mwendokasi 509 ambapo pia walikamata Pikipiki na Bajaji kwa makosa hayo 786.
Kamanda amewashukuru wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kwa kuendelea kutoa taarifa za uhalifu, na kuwaomba waendelee hivyo hivyo ili wahalifu wakamatwe na kuchukuliwa hatua, hali ambayo itadumisha Amani na utulivu na mkoa kuendelea kuwa salama.
Pikipiki zikiwa zimekamatwa ambazo zilikuwa zikitumika katika matukio ya makosa mbalimbali.
Nondo za wizi.
Viti vya wizi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464