RC MNDEME ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI NYAHANGA MANISPAA YA KAHAMA NA KUZITATUA
Na Marco Maduhu,KAHAMA
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amesikiliza kero za wananchi wa Kata ya Nyahanga Manispaa ya Kahama na kuzitatua.
Mkutano huo umefanyika leo Septemba 20,2023 katika Mtaa wa Shunu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, akiwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Thomas Muyonga wakisikiliza kero za wananchi.
Amesema kero ambazo zimewasilishwa na wananchi Serikali imezisikia na itazifanyia kazi,na kuwaagiza viongozi wote wa Kahama akiwamo na Mkuu wa wilaya hiyo Mboni Mhita kuzishughulikia utatuzi wake.
"Kero ambazo mmeziwasilisha wananchi nimetoa maelekezo kwa wasaidizi wangu watazifanyia kazi na zote zitashughulikiwa," amesema Mndeme.
Aidha, amesema kwa upande wa kero za maendeleo, baadhi zimeshaanza kutekelezwa ikiwamo ya ubovu wa miundombinu ya barabara, na fedha zinaendelea kutolewa ili kuendelea na ujenzi katika maeneo mengine.
Amesema katika Mkoa wa Shinyanga, Rais Samia ametoa kiasi cha fedha Sh.Trilioni Moja ndani ya utawala wake ambazo zitatumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Amewaagiza pia viongozi kutatua matatizo ya migogoro ya ardhi kwa kuzingatia utoaji wa haki kero ambayo imekuwa tatizo kubwa, huku akimwagiza Mkurugenzi kumalizia ujenzi wa Zahanati ya Shunu.
Mndeme amewasihi pia wananchi waendelee kumuunga Mkono Rais Samia ili aendelee kuwatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, huku akiwataka katika chaguzi zijazo wachague wagombea wote wanaotoka CCM.
Nao baadhi ya wananchi wakiwasilisha kero zao kwenye Mkutano huo, walilalamikia tatizo la migogoro ya ardhi, ikiwamo na ulipwaji fidia, ubovu wa miundombinu ya barabara, maji, na tatizo la umeme, kero ambazo Mkuu wa Mkoa alizitolea majibu ya utatuzi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza na wananchi wa Nyahanga kwenye Mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero zao na kuzitatua.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita akiendelea kuzungumza kwenye Mkutano huo wa hadhara.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Thomas Muyonga akizungumza kwenye Mkutano huo wa hadhara.
Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Wananchi wakiendelea na Mkutano na kusikiliza utatuzi wa kero zao.
Mwananchi Monica Charles akiwasilisha kero kwenye Mkutani wa hadhara.
Mkutano ukiendelea.
Wananchi wakiendelea na Mkutano.
Mwananchi Kassimu Masuka akiwasilisha kero kwenye Mkutano huo wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Mkutano ukiendelea.
Wananchi wakiendelea na Mkutano.
Burudani ikitolewa kwenye Mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, akiwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita akiburudika kwenye Mkutano huo na wachezaji wa Ng'anakang'wa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464