AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA KUKUTWA NA KOSA LA KUMNAJISI MTOTO MIAKA 8 KAHAMA


Na Kareny Masasy,

Kahama.

MAHAKAMA ya wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga imemuhukumu Mkazi wa Kijiji Cha Chapulwa kata ya Mwendakulima Kaliyango Maganga (55) kifungo cha maisha jela kwa kukutwa na kosa la kumnajisi mtoto mwenye umri wa miaka nane 8) anayesoma darasa la kwanza.

Hakimu mkazi wa mahakama hiyo Christina Chovenye jana alitoa hukumu hiyo iliyokuwa kesi jinai namba 240/2023 ambapo mshtakiwa ilidaiwa alitenda kosa hilo mara kwa mara kwa mtoto huyo nakushtakiwa tarehe 30/07/2023.

Hakimu Chovenye alisema mshtakiwa alikuwa na kazi ya umwagiliaji bustani ya maua nyumba ya jirani na mtoto huyo ambapo alikuwa akimvizia wakati akienda shule walezi wake wakimuacha peke yake nakwenda kwenye Shughuli za uchimbaji madini katika Mgodi wa Mwime.

"Walezi wake ambazo babu na Bibi walikuwa wakiondoka nakumuacha ndipo mtuhumiwa alikuwa akimchukua na kumnajisi huku akimueleza asimwambie mtu akisema atamuua"alisema Chovenye.

Hakimu Chovenye alisema mtoto mwenyewe alisikilizwa na kutoa maelezo ya kunajisiwa na mtuhumiwa mara kwa mara na vipimo vya daktari vimethibitidha hivyo mahakama haikuwa na shaka lolote juu ya utoaji wa hukumu hiyo dhidi ya mshtakiwa.

Hakimu Chovenye alisema walimu wa shule anayosoma mtoto huyo walitoa maelezo ya kugundua mtoto huyo kunajisiwa nakueleza kila siku amekuwa akichelewa shule na akifika anakuwa amechoka na kuwa na maumivu makali.

Mwendesha mashtaka ambaye ni wakili wa Serikali Evodia Baimo alisema kesi hiyo imesikilizwa mara nne tangu kufunguliwa kwa shauri hilo na wamesikiliza na adhabu kwa mshtakiwa iko sahihi ili owe fundisho kwa wengine.

Mshtakiwa Kaliyango Maganga akijitetea kwa upande wake aliomba kupunguziwa adhabu hiyo kwa madai ni mzee na anategemewa na familia.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464