RC MNDEME ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI KIJIJI CHA BUGELA WILAYANI KAHAMA
Na Marco Maduhu,KAHAMA
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme amesikiliza kero za wananchi katika Kijiji cha Bugela Kata ya Ulowa Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama na kuzitolea majibu.
Mkutano huo wa kusikiliza kero za wananchi wa Kijiji hicho cha Bugela umefanyika Septemba 18,2023 katika Kitongoji cha Kasheshe.
Wananchi wakiwasilisha kero zao kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, walilalamikia tatizo la ukosefu wa mawasiliano ya simu, ucheleweshaji wa Ruzuku ya Mbolea na kuchelewa kulipwa malipo ya mauzo ya Tumbaku.
Kero zingine ambazo wamezitaja ni uchache wa shule na kusabisha wanafunzi kusoma kwa msongamano darasani, umaliziaji wa maboma ya Zahanati yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi.
Wametaja pia ubovu wa miundombinu ya barabara, ukosefu wa huduma ya umeme, maji, hakuna kituo cha Polisi na kusabisha ukosefu wa amani, huku wakiomba pia kuruhusiwa kulina hasari katika eneo la maliasili la usumbwa
Naye Mkuu wa Mkoa akijibu kero hizo amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia, imetoa pesa nyingi mkoani humo zaidi ya Sh.Trilioni moja kwa ajili ya kutekelezwa miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwano Sekta ya Elimu, Afya, Barabara, Maji na Nishati.
Amesema kwa upande wa ukosefu wa mawasiliano tayari Kampuni ya Simu za Mkononi Vodacom walishafika kijiji humo ili kutatua tatizo hilo, kwa upande wa Ruzuku ya Mbolea ameagiza isicheleweshwe tena kwa Wakulima na huduma hiyo wasogezewe kwa ukaribu na siyo kuwekwa mbali nao.
Akizungumzia suala la malipo ya fedha za Tumbaku amesema tayari ameshatoa maagizo hadi kufikia siku ya ijumaa Kampuni zote ambazo zinadaiwa fedha na wakuli ziwe tayari zimewalipa kabla ya kuwachukulia hatua.
Amesema kwa upande wa ukosefu wa Amani tayari ameshatoa maagizo kwa Jeshi la Polisi kulifanyia kazi suala hilo, huku akiwataka Wananchi kuacha tabia ya kukaa na wahamiaji harafu kiholela bali wafuate taratibu za kupata kibali uhamiaji sababu wahalifu ambao wapo katika maeneo hayo ni wahamiaji haramu ambao wengine hufanya kazi kwenye mashamba ya Tumbaku.
Aidha Mndeme akizungumzia umaliziaji wa maboma ya Zahanati amesema Serikali itayakamilisha kwa awamu huku akitoa ahadi ya mifuko 100 ya Saruji ilikukamilisha ujenzi wa Zahanati kijijini humo.
Katika hatua nyingine Mndeme amewataka wananchi kuchukua tahadhari ya mvua ambazo zinatarajiwa kuanza kunyesha mwezi ujayo za Elinino kwamba kwa wale ambao wanaishi mabondeni waanze kuhama.
Naye Mbunge wa Ushetu Emmanule Cherehani amesema kero nyingi ambazo zilikuwa jimboni humo zimetatuliwa na kusalia chache ambazo nazo zipo kwenye utekelezaji.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Thomas Muyonga, amesema kwamba katika wilaya hiyo wameridhika na utekelezaji wa ilani ya CCM chini ya Rais Samia sababu matatizo mengi ambayo yalikuwa yakiwakabili wananchi yametatuliwa, huku akiwasihi wananchi waendelee kumuunga mkono Rais Samia.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi katika Kijiji cha Bugela Kata ya Ulowa.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kahama Thomas Muyonga akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mbunge wa Ushetu Emmanuel Cherehani akizungumza kwenye Mkutano huo.
Diwani wa Ulowa Gambriela Kimaro akizungumza kwenye Mkutano huo.
Viongozi wa CCM wakiwa kwenye Mkutano huo.
Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na kuwasilisha kero zao.
Mwananchi Anjela Shigemo akiwasilsha kero akiwasilisha kero kwenye Mkutano wa Mkuu wa Mkoa.
Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa Mkuu wa Mkoa.
Wananchi wakiendelea kuwasilisha kero zao kwenye Mkutano huo.
Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa Mkuu wa Mkoa.
Wananchi wakiendelea kuwasilisha kero.
Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa Mkuu wa Mkoa.
Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa Mkuu wa Mkoa.
Mwananchi Malulu Njamba Malulu akiwasilisha kero.
Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa Mkuu wa Mkoa.
Wananchi wakiendelea kuwasilisha kero.
Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa Mkuu wa Mkoa.
Mkuu wa Oparation Kilimo kutoka Kampuni ya ununuzi wa zao la Tumbaku Kampuni ya Mkwawa Godfrey Gobo akijibu malalamiko ya wakulima kuwachelewwsha kulipa fedha zao.
Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa Mkuu wa Mkoa.
Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa Mkuu wa Mkoa.
Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa Mkuu wa Mkoa.
Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa Mkuu wa Mkoa.
Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa Mkuu wa Mkoa.
Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa Mkuu wa Mkoa.
Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa Mkuu wa Mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akikabidhi Jezi kwa viongozi wa timu za mpira wa miguu kutoka Kijiji cha Ngilimba na Bugela.
Picha ya pamoja ikipigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464