TPDC,IMETOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA MRADI BOMBA LA MAFUTA ‘EACOP’, GESI ASILIA
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), wametoa mafunzo kwa waandishi wa habari mkoani Shinyanga,kufahamu Mradi wa Bomba la kusafisha Mafuta Ghafi (EACOP) na Gesi Asilia.
Mafunzo hayo yametolewa leo Septemba 26,2023 na kufunguliwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC Marie Msellemu, amesema wanatoa mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka Mikoa Nane, ambapo unapita mradi huo wa bomba la kusafisha mafuta Ghafi, ili wawe na uelewa zaidi juu ya maendeleo ya ujenzi wa bomba hilo.
Amesema waandishi wa habari wakielewa maendeleo ya mradi huo wa bomba la mafuta,watatumie vyema Kalamu zao kuelimisha jamii, pamoja na kuondoa upotoshaji ambao umekuwa ukivumishwa kwamba mradi huo umesimama.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC Marie Msellemu.
"Mafunzo kama haya ambayo tumeyatoa kwa waandishi wa habari Shinyanga, tutatoa pia katika mikoa mingine ambapo mradi huu unapita ili wafahamu hutua ambazo zimefikiwa za utekelezaji wa mradi huu wa bomba la mafuta," amesema Mselemu.
Naye Mratibu wa Mradi wa Bomba la Mafuta Kitaifa Asiadi Mrutu, amesema utekelezaji wa mradi huo hadi sasa umefikia asilimia 25,na wameshalipa fidia wananchi 9,813 sawa na asilimia 99 kiasi cha bilioni 34.8.
Mratibu wa Mradi wa Bomba la Mafuta Kitaifa Asiadi Mrutu.
Amesema kwa upande wa ujenzi wa bomba lenyewe la kusafisha Mafuta Ghafi ndiyo wapo kwenye maandalizi ya ujenzi, na walikuwa wakijenga makambi, karakana ya mabomba na Matenki ya mafuta ambayo asilimia kubwa yamekamilika.
Kwa upande wake Mgeni Rasmi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi, amewataka waandishi wa habari mafunzo hayo wayatumie vyema kutoa elimu sahihi kwa wananchi juu ya maendeleo ya mradi huo wa bomba la mafuta.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi.
Naye Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Shinyanga (SPC) Grayson Kakuru, akizungumza kwa niaba ya waandishi wa habari mkoani humo, amesema mafunzo hayo yatawaongeza ufanisi katika utendaji wao kazi.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Shinyanga (SPC) Grayson Kakuru.
Afisa Mahusiano Mradi wa Bomba la Mafuta (EACOP)Catherine Mbatia akizungumza kwenye Mafunzo hayo.
Afisa Mawasiliano Mradi wa Bomba la Mafuta (EACOP) Abbas Abraham akizungumza Mafunzo hayo.
Viongozi wakiwa Meza kuu.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.
Mafunzo yakiendelea.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464