RC MNDEME AKAGUA UJENZI WA BARABARA AMBAZO ZINAJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI KAHAMA
Na Marco Maduhu, KAHAMA
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amekagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya Barabara ambazo zinajengwa kwa kiwango cha Lami katika Mitaa ya Manispaa ya Kahama, huku akiagiza kasi iongezeke ili zianze kutumika.
Amefanya ziara hiyo leo Septemba 20,2023 kwa kukagua barabara hizo zikiwa na jumla ya Kilomita 1.3 zenye thamani ya Sh.bilioni 1.2.
Amesema katika ujenzi wa Barabara hizo hakuna Mkandarasi kuongezwa muda sababu fedha zipo na anapaswa kukamilisha ndani ya muda na kiwango chenye ubora.
"Awamu ya kwanza ya ujenzi wa miundombinu hii ya barabara kwa kiwango cha lami ukamilike Oktoba,na awamu ya Pili ukamilike Januari 2024 sababu pochi la mama limefunguka na fedha zipo na hakuna kilichosimama," amesema Mndeme.
Aidha, amewataka wananchi waitunze miundombinu hiyo ya barabara na kuacha kutupa uchafu kwenye mitaro ili isizibe.
Naye Mkandarasi ambaye anatekeleza ujenzi wa miundombinu ya barabara hizo kwa kiwango cha lami Manispaa ya Kahama Hajoka International Company Johansen Kajuna ameahidi kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.
Kawa upande wake Kaimu Meneja Wakala wa Barabara Mjini na vijijini (TARURA) wilaya ya Kahama Mhandisi Masolwa Juma, akisoma taarifa ya ujenzi wa barabara hizo amesema zina urefu wa kilomita 1.39 na zinathamani ya Sh.bilioni 1.2 za zinatekelezwa kwa awamu mbili.
Nao baadhi ya wananchi wa Kahama wamepongeza ujenzi wa barabara hizo kwa kiwango cha lami, ambapo licha ya kupendezesha mji zitachochea ukuaji wa uchumi na kutoharibu vyombo vyao vya moto mara kwa mara sababu ya ubovu wa barabara.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa Barabara kwa Kiwango cha Lami.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464