RC MNDEME ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI WA BULIGE NA KUZITOLEA MAJIBU

RC MNDEME ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI WA BULIGE NA KUZITOLEA MAJIBU

Na Marco Maduhu, KAHAMA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amefanya Mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi wa Kata ya Bulige Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama na kuzitolea majibu.

Mkutano huo wa hadhara umefanyika leo Septemba 19,2023 katika eneo la Mnada uliopo Center ya Bulige.
Mndeme akijibu kero mbalimbali za wananchi likiwamo Tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara na kushindwa kufanya shughuli za maendeleo ikiwamo na kusaga nafaka, ameiagiza TANESCO kutoa ratiba kwa wanachi ya kukatika kwa umeme huo, wakati Serikali ikiendelea kulitatua sababu ni tatizo la nchi nzima.

Amesema katika utatuzi wa kero mbalimbali Rais Samia ametoa fedha nyingi za kutekelezwa miradi ya maendeleo, na kwamba katika Mkoa wa Shinyanga ametoa kiasi cha Sh.Trilioni 1, ambapo kwa Halmashauri ya Msalala pekee Sh,bilioni 7 na Kata ya Bulige Sh.bilioni 1, na kuwataka wananchi wamuunge Mkono Rais Samia ili aendelee kuwaletea maendeleo.
“Kero zote ambazo mmeziwasilisha hapa Pochi la Mama limefungaka na zote zitatatuliwa,”amesema Mndeme.

Pia amewapongeza wananchi hao kwa kuchagia ujenzi wa miradi ya maendeleo na hata kuanzisha ujenzi wa maboma yakiwamo ya Zahanati, na kuahidi Serikali itayakamilisha yote na kupata huduma.

Katika hatua nyingine Mndeme amewataka wananchi waitunze Amani ya Nchi na kuacha kupokea wageni hovyo ambao hawawajui, huku akiwatadharisha pia wachukue tahadhari mapema juu ya mvua kubwa ambayo imetangazwa kunyesha na wananchi ambao wanaishi mabondeni waanze kuhama, pamoja na kuitumia mvua hiyo kulima mazao hasa ya Mpunga.
Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kahama Thomas Muyonga akizungumza kwenye Mkutano huo, amesema CCM waliahidi na sasa kero nyingi zimetatuliwa ,na kuwataka wananchi waendelea kuwa na Imani na Chama hicho ambacho ndicho chenye kuwaletea maendeleo.
Nao baadhi ya wananchi wakiwasilisha kero zao kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, walilalamikia tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara na umaliziaji ujenzi wa Maboma ambayo yamekuwa yakianzishwa kwa nguvu za wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza na wananchi wa Bulige kwenye Mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero zao na kuzitatua.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Thomas Muyonga akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mhandisi kutoka TANESCO Kahama Onesy Mbembe akitoa majibu kwa wananchi juu ya tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara kwenye Mkutano huo wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Wananchi wa Bulige wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Mwananchi akiwasilisha kero kwa Mkuu wa Mkoa.
Wananchi wa Bulige wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464