RC MNDEME AWAPONGEZA WANANCHI KUANZISHA UJENZI SHULE MPYA YA SEKONDARI NYAHANGA MANISPAA YA KAHAMA

RC MNDEME AWAPONGEZA WANANCHI KUANZISHA UJENZI SHULE YA SEKONDARI NYAHANGA MANISPAA YA KAHAMA

Na Marco Maduhu,KAHAMA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amewapongeza wananchi wa Nyahanga Manispaa ya Kahama, kwa kujitoa kuchangia shughuli za maendeleo na kuanzisha ujenzi wa shule mpya ya Sekondari, na kuwaondolea adha wanafunzi kutembea umbali mrefu.

Mndeme amebainisha hayo jana wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo mpya ya Sekondari Nyahanga, ambayo imeanzishwa kwa nguvu za wananchi kwa kujenga vyumba 6 vya madarasa, ambapo Serikali imeongeza vyumba 8 na kufikisha vyumba 14 ambapo uhitaji ni vyumba 16 na kusalia viwili.
Amesema ni jambo jema wananchi kujitoa kuchangia shughuli za maendelo ikiwamo kuanzisha ujenzi wa shule mpya, na kumuunga mkono Rais Samia kukuza sekta ya elimu hapa nchini, na kuwahidi kuwa Serikali itaikamilisha shule hiyo na mwakani kuanza kutoa elimu kwa wanafunzi.

“Katika taarifa ya ujenzi wa shule hii uhitaji ni madarasa 16, ambapo wananchi wamejenga 6 na Serikali 8 na kusalia mawili, na kuagiza Mkurugenzi malizia haya madarasa mawili ili wanafunzi wasome katika mazingira mazuri na kufanya vizuri kitaaluma,”amesema Mndeme.
“Kata hii ya Nyahanga nimeambiwa kuna shule 10 za msingi, hivyo shule hii moja haitoshi, wakati wanafunzi wakiendelea kusoma katika shule hii, anzisheni tena ujenzi wa shule nyingine,”ameongeza Mndeme.

Katika hatua nyingine Mndeme, ameiagiza Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Kahama (KUWASA), kupeleka huduma ya maji shuleni hapo, TARURA kuchonga barabara nzuri pamoja na TANESCO kupeleka huduma ya Umeme.
Naye Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Kahama Anastazia Vicent, akisoma taarifa ya ujenzi wa shule hiyo, amesema umefika asilimia 45 na hadi kufikia Oktoba utakuwa umekamilika, na mwakani itaanza kutoa elimu kwa wanafunzi 831 wa kidato cha kwanza.

Amesema katika ujenzi wa Shule hiyo Serikali imetoa Sh.milioni 603.8, na Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani (2023/2024) imetenga Sh,milioni 99 na wanafunzi watasoma karibu na siyo kutembea tena umbali wa kilomita 14 kwenda shule ya Sekondari Seke iliyopo Zongomela.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akishiriki kwenye ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Nyahanga Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akishiriki kwenye ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Nyahanga Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akishiriki kwenye ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Nyahanga Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akishiriki kwenye ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Nyahanga Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akisalimiana na mafundi ambao wanajenga shule mpya ya Sekondari Nyahanga Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita akishiriki kwenye ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Nyahanga Manispaa ya Kahama.
Muonekano wa shule mpya ya Sekodari Nyahanga Manispaa ya Kahama.
Muonekano wa shule mpya ya Sekodari Nyahanga Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiwa katika ziara ya kukagua ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Nyahanga.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464