BSL YAITAKA JAMII KUTOWAKATISHA WATOTO WALIORUDI KUSOMA KATIKA MFUMO WA NJE YA ELIMU


Wanafunzi walio kwenye programu ya SEQUIPE wanao simamiwa na tassis ta BSL waki katika ofisi ya Afisa elimu mkoa wa Shinyanga

Na Kareny Masasy,Shinyanga

MKURUGENZI wa taasisi za BSL hapa nchini Frank Peter (Mr Black) ambayo inahusika na huduma ya utoaji wa haki elimu kwa watoto waliokatiza masomo kutokana changamoto mbalimbali ameiomba jamii kutowakatisha tamaa watoto ambao wameanza kusoma kupitia mfumo wan je ya Elimu.


Mkurugenzi huyo amesema haya jana mbele ya Afisa elimu mkoa wa Shinyanga Dafrosa Ndalichako akiwa ameambatana na wanafunzi hao wanaosoma kupitia mfumo huo.

Peter amesema ni mwaka wa pili sasa tangu waanze kuendesha programu ya SEQIPE inayoendeshwa na serikali kwaajili ya kuwakomboa watoto wa kike na yeye kusimamia kupitia taasisi yake yenye vituo tisa hapa nchini.

“Tumekuwa tukitoa Elimu katika mfumo huria na masafa na mfumo wa elimu ya sekondari mbadala kwa mwaka wa tisa sasa lengo kuwasaidia watoto wa wakike walioshindwa kufikia elimu ya sekondari” amesema Peter.

Ameipongeza serikali na kuishukuru kwa kutoa mchango wa kuwalipa walimu fedha za kujikimu hivyo nao wanajitahidi kurudisha saikolojia ya wanafunzi ili kurudisha moyo na molari ya usomaji wasianguke tena.

“Kwa Manispaa ya Kahama waliweza kusajili watoto 265 na mpaka sasa kuna watoto 23 na Manispaa ya Shinyanga waliosajili watoto 81 lakini mpaka sasa wapo 26 changamoto iliyopo watoto kukatishwa ikiwemo pia kutembea umbali mrefu mikakati iliyopo kujengwa kw hosteli ili kusiwemo changamoto ya kukatisha tena masomo”amesema Peter.

Dedan Rutazika Afisa elimu watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi amesema kuna maadhimisho ya elimu ya watu wazima ambayo yameanza kuadhimishwa wiki hii yakiwa na kauli mbiu kukuza uwezo wa kusoma na kuandika kwa ulimwengu unaobadilika kujenga misingi ya jamii endelevu na yenye amani.

Kauli mbiu hii inatufanya kuona umuhimu wa kusimamia haki ya binadamu ya msingi ya kupata Elimu kwa watu wote na maadhisho haya yameanza katika ngazi za halmashauri na wananchi wanahimizwa kujiunga na elimu ya watu wazima.

Rutazika amesema vipo vituo vilivyoanzishwa vya kuendeeza elimu ambapo kuna watoto wa kike 166 ambao wanaendelea kupata masomo kupitia programu ya SEQUIP walikatisha masomo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kupata mimba .

Sambamba na hilo pia mkurugenzi wa tasisi ya BSL alitembelea chuo cha serikali za mitaa kampasi ya Shinyanga nakukutana na mshauri wa chuo hicho Mkwamila Charles ambaye aliwatia moyo wanafunzi kusoma kwa bidii ili wapate ufaulu wakujiunga na chuo hicho.

Mkurugenzi wa BSL akiwa ameambatana na wanafunzi hao alikutana na kamanda wa polisi mkoani hapa Janeth Magomi nakuelezea wao wamekuwa wakipinga vitendo vya ukatili kupitia dawati la jinsia hivyo dawati hilo walitumie kuripoti vitendo vya ukatili vinavyofanyika.

Wanafunzi walipotembelea chuo cha serikali za mitaa kampasi ya Shinyanga.

Wanafunzi waliokatika Elimu ya programu nje ya mfumo rasmi wa Elimu kutoka taasisi ya BSL manispaa ya Shinyanga


Afisa elimu ya watu wazima mkoani Shinyanga Daden Rutazika akiwa ofisini tayari kuwapokea wanafunzi hao walipotembelea ofisi za Elimu

Mkurugenzi wa taasisi ya BSL nchini Frank Peter (Mr Black) akiongea kuhusu wanafunzi hao

Mshauri wa wanafunzi Mkwamila Charles kutoka chuo cha serikali za mitaa kampasi ya Shinyanga akiwashauri wanafunzi na kuwapa nasaha za kusoma kwa bidii

Wanafunzi wakiwa wamemabatana na mkurugenzi wa BSL kwenye ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464