RC MNDEME AFUNGUA ZAHANATI YA SESEKO, AONYA UPOTEVU WA DAWA.
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme,amefungua Rasmi Zahanati ya Seseko iliyopo Kata ya Mwamalili Manispaa ya Shinyanga,huku akionya kusitokee upotevu wowote wa dawa.
Amezindua Zahanati hiyo leo Septemba 25,2023 wakati alipofanya ziara ya kutembelea utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Manispaa ya Shinyanga.
Amesema Rais Samia katika Mkoa wa Shinyanga ametoa fedha nyingi za kuboresha huduma za Afya, ili wananchi wapate huduma bora za matibabu, na kuwataka watumishi watoe huduma stahiki na kusitokee wizi wowote wa dawa.
"Leo nimeifungua Rasmi Zahanati hii ya Seseko kutoa huduma za matibabu kwa wananchi, naagiza kusitokee upotevu wowote wa dawa hata Panadol, na dawa hizi ziwafikie walengwa," amesema Mndeme.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa akiweka Jiwe la Msingi ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa dharura Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga, amewaonya pia watumishi wa Afya kuacha tabia ya kuchati na simu wala kucheza game wakati wakitoa huduma za matibabu kwa wagonjwa.
Pia, amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze, kuhakikisha katika Hospitali hiyo kuwepo na 'Standby Generator' ili umeme ukikatika wagonjwa waendelee kupata huduma za matibabu na kuokoa Afya zao.
Naye Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Seseko Dk.Briliance Ombay, akisoma taarifa ya ujenzi wa Zahanati hiyo amesema umegharimu Sh.milioni 95.6 na inatoa huduma za matibabu kwa wananchi 2,741.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga Dk. Pierina Mwaluko, amesema Serikali imetoa kiasi cha fedha Sh.milioni 500 kujenga jengo hilo na hadi sasa wameshatumia milioni 292.
Nao baadhi ya Wananchi wa Shinyanga, wameishukuru Serikali kwa kuwaboreshea upatikanaji wa huduma za Afya kwa kujenga Hospitali pamoja na upatikanaji wa madawa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza mara baada ya kufungua Zahanati ya Seseko.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiwa katika Zahanati ya Seseko.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akifungua Zahanati ya Seseko.
Muonekano wa Zahanati ya Seseko.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kushoto)akiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi katika Stoo ya Madawa Zahanati ya Seseko.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiwa katika ujenzi wa Jengo la wagonjwa wa dharura katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiweka Jiwe la Msingi katika ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa dharura katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akikagua ujenzi wa jengo la wagonjwa wa dharura katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464