Mjumbe wa UWT kwenda halmashauri kuu ya Wilaya Mariam Kajala akiwashukuru wajumbe baada ya kumchagua
Suzy Luhende Shinyanga press blog
Umoja wa wanawake UWT Wilaya ya Shinyanga mjini leo umefanya uchaguzi wake mdogo wa kuziba nafasi iliyokuwa wazi ya mjumbe wa kutoka UWT kwenda halmashauri kuu ambapo alifanikiwa kuibuka kidedea Mariam Kajala kati ya wagombe wanne waliokuwa wakiwania nafasi hiyo.
Uchaguzi huo umefanyika leo katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini ambao msimamizi mkuu wa uchaguzi huo alikuwa mjumbe wa baraza UWT Taifa Christina Gule na Mery Mpazi mjumbe wa baraza la UWT Mkoa.
Msimamizi mkuu wa uchaguzi huo Gule amesema wapiga kura walikuwa 54 Wagombea walikuwa wanne ambao ni Matha Nzuku hakupata kura, Theonestina Martine hakupata kura, Mery Izengo alipata kura 22 na Mariam Kajala alipata kura 32 ambaye ndiye aliibuka mshindi.
"Tumeanza uchaguzi wetu kwa utulivu na amani na tumemaliza kwa utulivu hivyo nikuombe kiongozi uliyechaguliwa ukashirikiane vizuri na viongozi wenzako katika kuhakikisha CCM inapata ushindi wa kishindo niwaombe wagombea wengine ambao kura hazikutosha msikate tamaa hapa tumepangana tu tuendelee kushirikiana katika kufanya kazi za Chama,"amesema Gule.
Kwa upande wake Mwemyekiti wa UWT Shinyanga mjini Rehema Nhamanilo amewataka wajumbe wote kuondoa makundi yaliyokuwepo kwa ajili ya uchaguzi huo badala yake wawe na kundi moja la CCM pekee na kuwa na umoja katika kuitumikia jumuiya na Chama.
Naye kaimu katibu wa UWT wilaya Naibu Katalambula ambaye ni katibu wa vijana amesema wamefanya uchaguzi wa haki na wa amani ambao ulikuwa wa wazi hivyo hakuna wa kulalamika kuwa hajatendewa haki hivyo wakiopata na ambao hawajapata waendelee kukitumikia chama kwa ushirikiano mkubwa kwani wote ni wamoja katika chama.
Awali kabla ya kuanza uchaguzi mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Shinyanga Grace Samweli Bizuli aliombea uchaguzi na kuwataka wafanye uchaguzi kwautulivu kwani kiongozi anapangwa na Mungu anatehitajika ni mmoja hivyo atakayepatikana ashirikiane na viongozi wenzake.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi amewapongeza viongozi kwa kufanya uchaguzi kwa utulivu na kuwataka viongozi wote wahakikishe kesho watoto wote wanaofanya mtihani wa darasa la saba wanaenda shule kufanya mtihani huo.
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini Rehema Nhamanilo akizungumza baada ya uchaguzi kuisha
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Shinyanga Grace Samweli Bizuri akizungumza
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Naibu Katalambula akizungumza ambaye alikuwa kaimu katibu wa UWT
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha uchaguzi mdogo
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha uchaguzi mdogo
Viongozi wa UWT mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na wagombea na viongozi mbalimbali wa kata
Viongozi wa UWT mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na wagombea na viongozi mbalimbali wa kata
Viongozi wa UWT mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na wagombea na viongozi mbalimbali wa kata
Wajumbe wa kikao cha baraza wakiwa kwenye kikao cha uchaguzi mdogo