WANAWAKE WAASWA KUSIMAMIA MALEZI NA MAKUZI KWA NJIA YA IMANI
Wanawake wa kansia la IEAGT kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wakiwa katika kongamano la kitaifa la kanisa hilo
Na Elizabeth Nyanda.
Ili kupambana na kasi ya mmomonyoko wa maadili katika jamii Wanawake wametakiwa kusimamia malezi ya watoto kiimani(kiroho) kama sehemu ya kuandaa kizazi chenye maadili mema na chenye hofu ya Mungu.
Hayo yamesemwa septemba 14 ,2023 na mwenyekiti wa Umoja Wanawake Wa Injili (UWWI) wa kanisa la International Evangelical Assemblies of God Tanzania (IEAGT) ,Jimbo la Mwanza Anastasia Deonard wakati akizungumza katika kongamano la kitaifa la wanawake wa kanisa hilo mkoani Shinyanga.
Amesema wanawake wamekuwa bise kufukuzia pesa na kusahau jukumu la malezi hata wakienda kumwabudu Mungu wanawaacha watoto katika biashara au kulinda nyumba hali ambayo imekuwa ikichangia watoto kukosa msingi wa mafundisho ya ki Mungu ambayo ndio chanzo cha hofu ya Mungu.
"Wanawake tusiache watoto wetu nyumbani walandelande nakucheza ovyo twenden nao kwenye nyumba za ibaada nao wakajifunze neno la Mungu ili wakue wakijua ubaya wa dhambi itawanusuru na ghasia ya mmomonyoko wa maadili nao watakuwa waalimu wazuri baadae"amesema Anastasia
Katika hatua nyingine amesisitiza wanawake kuliombea Taifa katika nyanja mbalimbali ikiwemo watoto ambao ni Taifa na viongozi baadaye kwani ndio jukumu lao kibiblia .
Aidha, Mkurugenzi wa wanawake Taifa kanisa la (IEAGT) Suzan Mabushi akiwata wanawake kutokwepa jukumu la malezi kwa kuwapeleka watoto wao kulelewa na bibi au ndugu wengine jambo ambalo limekuwa likiharibu hatima ya watoto wengi.