Header Ads Widget

WAZAZI WATAKIWA KUWAFUNDISHA NENO LA MUNGU WATOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUKEMEA VITENDO VYA UKATILI


Wanawake wa kanisa la Philadelfia Miracle Temple wakiwa kwenye picha ya pamoja 

Suzy Luhende Shinyanga press blog

Wazazi na walezi wametakiwa kuwafundisha maadili mema ya kimungu watoto pamoja na kutenga muda wa kuwafundisha neno la Mungu ili waweze kulielewa na kuzungumza nao pindi wanaporudi kutoka kwenye shughuli zao, ili wasijiingize kwenye vitendo viovu visivyompendeza Mungu na jamii kwa ujumla.

Licha ya kufundisha maadili mema pia wazazi wametakiwa kukemea vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vinavyofanywa na baadhi ya watu katika jamii.



Hayo yamesemwa na Anna Lukas wakati akihubiri neno la Mungu kwenye sherehe ya wanawake iliyofanyika jumapili katika kanisa la Philadelfia Miracle Temple lililoko kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga, ambapo amewataka wazazi na walezi kuwafundisha maadili ya kimungu watoto ili wanapoendelea kuwa wakubwa wasifanye vitendo visivyompendeza Mungu.

Amesema wazazi wengi wamekuwa wakijisahau kuwafundisha maadili mema ya kimungu watoto hali ambayo imekuwa ikisababisha watoto kujiingiza kwenye vitendo viovu na wengine kufanyiwa ukatili wa kijinsia na wengine kufanyiana wao kwa wao bila kujua kama ni vibaya.

"Niwaombe wazazi na walezi tuwalee watoto wetu katika malezi yanayotakiwa tusijisahau na shughuli zetu tutaharibu kizazi chetu tukae na watoto wetu tuzungumze nao tuwafundishe madhara ya urawiti, ushoga usagaji na ukatili mbalimbali wa kijinsia tukifanya hivyo watoto wetu watakuwa na uelewa nao watafundishana yaliyomema"amesema Anna

Aidha katika siku hiyo Anna alifundisha ukarimu wa kanisa ambapo aliwataka waumini wote kuwa na ukarimu, ambapo amesema apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu na atavuna vingi na Mungu atamfanikishwa.

"Waebrania 13: 2 inasema msisahau kuwafadhili wageni, maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua, lakini pia tunapowakaribisha majumbani kwetu tusiwachanganye na watoto wetu tuwape chumba chao cha kulala"amesema Anna

Pia wazazi wametakiwa kukemea ukatili wa aina mbalimbali na kuacha kuwafanyia ukatili watoto wao badala yake wawafundishe kwa upole, inapobidi kuwachapa kwa utaratibu unaotakiwa sio kuwatukana matusi makali kwani kufanya hivyo ni kuwafundisha ukatili watakaoufanya wao kwa baadae.
Mchungaji wa kanisa la Philadelfia Miracle Temple Baraka Laizer akizungumza baada ya sherehe ya wanawake wa kanisa hilo

Ma mchungaji wa kanisa la Philadelfia Miracle Temple Evarine Msangi akiwashukuru wanawake kwa kufanikisha sherehe yao
Wanawake wa Philadelfia Miracle Temple wakitoa sadaka kwa mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Baraka Laizer na mama mchungaji Evarine Msangi 
Mwenyekiti wa Philadelfia Miracle Temple Dionisia Kaijage akitoa zawadi kwa mchungaji msaidizi wa kanisa hilo Ananania Clement kwa niaba ya wanawake wa kanisa hilo

Mchungaji Anania akizungumza baada ya ibada ya wanawake kuisha 

Wanawake wa kanisa la Philadelfia Miracle Temple Dionisia Kaijage akitoa zawadi kwa mchungaji msaidizi wa kanisa hilo Ananania Clement kwa niaba ya wanawake wa kanisa hilo
Anna akihubiri neno la Mungu katika siku ya wanawake 

Viongozi wa wanawake wa kanisa la Philadelfia wakiwa kwenye picha ya pamoja kanisani hapo

Mmoja wa wanawake akisoma risala ya wanawake wa kanisa hilo

Wanawake wakiingia kanisani kwa ajili ya kuanza ibada 
Baadhi ya wanawake wakiwa kwenye picha ya pamoja kanisani hapo baada yaibada
Waumini wa kanisa hilo wakiendelea na mafundisho ya neno la Mungu katika ibada ya sherehe ya wanawake 



Post a Comment

0 Comments