NA EMMANUEL MBATILO
Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania bara wanaendelea kufanya ziara Kimataifa ambapo leo imefanikiwa kuinyuka Al-Merrikh 2-0 mchezo ambao umepigwa kwenye dimba la Pele Kigali nchini Rwanda.
Katika mchezo huo Yanga Sc imeweza kupata mabao kupitia kwa washambuliaji wao Kenned Musonda pamoja na Clement Mzize ambapo mabao yote yamefungwa kipindi cha pili.
Kwa upande wa majilani zao Simba Sc ambao walikuwa wanakipiga kule Ndola nchini Zambia wamelazimisha sare ya mabao 2-2, mabao ya Simba Sc yamefungwa na Mzambia Claotos Chama.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464