Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale Mhe. GRACE KINGALAM
E.
Na mwandishi wetu,
Katika
kuboresha wajibu wa wamiliki wa leseni za madini kwa jamii nchini (CSR)
Mgodi wa Barick bulyanhulu kwa kushirikiana na Tume ya madini Mkao mkuu
Wamefanya mafunzo ya kanuni mpya za CSR kwa Viongozi wa Halmashauri ya
Ngwang’hwale kwaajili ya kurahisisha Uaandaji na Utekelezaji wa miradi
Itakanayo na CSR.
Akieleza Umuhimu wa Mfunzo
hayo jana Mhandisi Migodi kutoka Tume ya Madini Mako makuu MACKENZIE MABULA
Amesema Awali kulikuwa na Sheria pekee zilizokuwa zinatumika ambapo
kulikuwa nachangamoto ya kuzielewa sharia zote hivyo ujio wa kanuni hizi
zitawarahisishia wasimamizi na watekelezaji wa miradi hiyo itokanayo na
CSR.
“Niseme tu ujio wa kanuni hizi
zitawasaidia sana katika uandaaji na utekelezaji wa miradi hii kuchambua
sharia moja baada ya nyingine kulikuwa nachangamoto zake lakini sasa
serikali yetu imeliona hilo sasa tutatumia kanuni niwaombe kwa pamoja
mgodi na halmashauri mkatekeleze ipasavyo miradi hiyo” –Mabula amesema
Meneja wa Mazingira na Mahusiano ya Mgodi wa Bulyanhulu
AGAPITI PAUL Ameiomba halmshauri hiyo kuendelea kushirikiana na mgodi
kwa kukamilisha miradi kwa wakati ili wananchi waweze kunufaika na
uwekezaji uliofanywa na mgodi huo wa Bulyanhulu .
“
Tujitahidi kumaliza kwa wakati miradi hii kwani lengo la mgodi na
serikali ni kuona wananchi wananufaika na wawekezaji nchini hasa sisi wa
madini ambao tumewekeza katika halmashauri yenu” –PAUL alisema.
Akifunga
mafunzo hayo kwa upande wa Halmashauri ya Nyang’hwale Mkuu wa wilaya
hiyo Mhe. GRACE KINGALAME Ameupongeza mgodi wa Barick bulyanhulu kwa
kuandaa mafunzo hayo kwani yatawasaidia waatalamu wake kutekeleza kwa
ufanisi Miradi hiyo itakayotolewa na Mgodi huo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464