MWENYEKITI WA CCM MKOA WA SHINYANGA MABALA MLOLWA ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI LYAMIDATI NA KUZITATUA
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, amesikiliza kero za wananchi wa Lyamidati wilayani Shinyanga na kuzitatua.
Amefanya Mkutano huo leo Oktoba 3,2023 akiwa ameambatana na Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum, Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa,Wilaya na Watalaamu kutoka Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Awali wananchi wakiwasilisha kero zao kwenye Mkutano huo wa Mwenyekiti CCM Mkoa, wamelalamikia tatizo la baadhi ya viongozi wa Kata hiyo kutofanya kazi zao kwa ufanisi, na wizi wa vifaa vya ujenzi katika Sekondari ya Ihugi.
Aidha, wameomba pia kukamilishiwa ujenzi wa Maboma ya Zahanati, kupelekewa Nishati ya Umeme,Maji ikiwamo na kwenye Taasisi za Serikali.
Mlolwa akijibu kero hizo amesema Serikali ya Rais Samia ni sikivu kwamba zote zitafanyiwa kazi, huku akiahidi kulishughulikia tatizo la wizi wa vifaa vya ujenzi Sekondari ya Ihugi kwa kupeleka wataalamu kufanya uchunguzi.
"Rais Samia amekuwa akitembea hadi nje ya nchi kwenda kutafuta pesa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo lakini watu wanakuja kuiba vifaa vya ujenzi, yani wote ambao mmehusika mtavirudisha," amesema Mlolwa.
Naye Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum, amesema katika jimbo hilo Rais Samia ametoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo,na vijiji vichache ambavyo vimesalia kupata huduma ya Maji na Umeme hadi kufikia 2025 kero hiyo haitakuwepo tena.
Amesema kwa upande wa Kata hiyo ya Lyamidati watapata umeme hivi karibuni pamoja na huduma ya Majisafi na Salama kutoka Ziwa Victoria.
Nao Wataalum wakijibu kero za wananchi akiwamo Kaimu Meneja wa Shirika la Umeme Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Ibrahimu Kiyungu, amesema katika Kata hiyo ya Lyamidati hadi kufikia Decemba mwaka huu umeme utakuwa umewaka.
Katika ziara hiyo ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, awali alikutana na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Kata ya Solwa na Lyabukande.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza na wananchi wa Lyamidati wilaya ya Shinyanga kwa kusikiliza kero zao na kuzitatua.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza na wananchi wa Lyamidati wilaya ya Shinyanga kwa kusikiliza kero zao na kuzitatua
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlowa (kushoto) akiwa na Mbunge wa Solwa Ahmed Salum kwenye Mkutano wa hadhara Lyamidati wilayani Shinyanga.
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Mkoa wa Shinyanga Richard Masele akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum akielezea miradi ya maendeleo ambayo ameitekeleza jimboni humo katika Mkutano huo wa hadhara Lyamidati.
Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum akiendelea kuzungumza kwenye Mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Edward Ngelela akizungumza kwenye Mkutano huo.
Diwani wa Lyamidati Veronica Mabeja akizungumza kwenye Mkutano huo.
Wataalamu wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye Mkutano huo kwa ajili ya kujibu kero za wananchi.
Mwananchi Hangwa Maporu akiwasilisha kero kwenye Mkutano huo.
Wananchi wakiendelea kutoa kero zao kwenye Mkutano huo.
Wananchi wakiendelea kutoa kero zao kwenye Mkutano huo.
Wananchi wakiendelea kutoa kero zao kwenye Mkutano huo.
Wananchi wakiendelea kutoa kero zao kwenye Mkutano huo.
Wananchi wakiendelea kutoa kero zao kwenye Mkutano huo.
Mtendaji wa Kata ya Lyamidati Joyce Mahina akijibu kero za wananchi.
Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Ibrahimu Kiyungu akijibu kero za wananchi.
Meneja wa TARURA wilaya ya Shinyanga Mhandisi Samson Pamhiri akijibu kero za wananchi.
Afisa kutoka RUWASA akijibu kero za wananchi.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Dk, Nuru Yunge akijibu kero za wananchi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa (kulia)katika ni Mwenezi wa CCM Mkoa Richard Masele na Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum wakitetea jambo kwenye Mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wananchi wa Lyamidati wilayani Shinyanga wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa wa kusikilizwa kero zao na kutatuliwa.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa (wapili kushoto)akiwa ziara Kata ya Lyamidati wilayani Shinyanga.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464