Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA)Mkoa wa Shinyanga wamehitimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kuendeleza Kampeni ya Uwajibikaji ya kutoa na kudai Risiti halali kwa Wafanyabiashara na Wananchi, ili Serikali ipate mapato sahihi, fedha ambazo zitatumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
TRA wamehitimisha wiki hiyo ya huduma leo Oktoba 6, 2023,ambayo ilianza Oktoba 3, kwa kufanya matembezi ya kutembelea baadhi ya Wafanyabiashara kwenye maduka yao na kuwapatia elimu ya kutoa Risiti halali kwa wateja, pamoja na kuzungumza na Wananchi juu ya umuhimu kudai Risiti halali za manunuzi ya bidhaa zao.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi ambaye alikuwa Mgeni Rasmi kwenye matembezi hayo, amewasihi Wafanyabiashara kuendelea kulipa kodi za Serikali kwa hiari na kutoa Risiti halali za mauzo ya bidhaa zao kwa wateja, pamoja na wananchi kudai Risiti halali, hali ambayo Serikali itapata mapato sahihi.
Amesema nchi yoyote ambayo imepiga hatua kimaendeleo wananchi wake ni walipaji wa kodi wazuri, na kuwasihi Wafanyabiashara wasikwepe kulipa mapato ya Serikali, bali walipe kwa hiari yao kwa maendeleo ya Taifa pamoja na kutoa Risiti halali za mauzo ya bidhaa zao kwa wateja na siyo kuiibia Serikali.
“Ulipaji kodi ndiyo msingi wa maendeleo ya Taifa letu, fedha ambazo zimekuwa zikipatikana ndizo hizi ambazo hutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo na miradi ya kimkakati,”amesema Samizi.
Aidha, amewataka pia wananchi kukataa tabia ya baadhi ya Wafanyabiashara kuwapatia Risiti za kusindikiza mzigo, ambazo hazina uhalisia wa kiwango halisi cha fedha ambazo wamenunua bidhaa zao na kuiibia mapato Serikali.
Naye Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga Faustine Mdessa, amesema wiki hiyo ya mlipa kodi wameitumia vizuri kutoa elimu kwa Wafanyabiashara na kutengeneza mahusiano mazuri, na kuwasihi juu ya ulipaji kodi kwa hiari na utoaji Risiti halali kwa wateja, fedha ambazo huwarudia kupitia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
“Faida ya utoaji na kudai Risiti halali ni kuisaidia Serikali kupata mapato sahihi,”amesema Mdessa.
Nao baadhi ya Wafanyabiashara mkoani Shinyanga akiwamo Warda Omary, wamesema wanafahamu faida za ulipaji kodi na wameona maendeleo makubwa ambayo yamekuwa yakifanywa na Rais Samia, na kutoa wito kwa Wafanyabiashara ambao hukwepa kulipa kodi na kutoa Risiti zisizo halali waache tabia hiyo kwa maendeleo ya Taifa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza na Wafanyabiashara kutoa elimu ya mlipa kodi na kutoa Risiti halali za
mauzo ya bidhaa kwa wateja.
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga Faustine Mdessa akielezea Kampeni ya uwajibikaji kutoa na kudai Risiti halali.
Mfanyabiashara Warda Omary akielezea namna wanavyolipa Kodi ya Serikali.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akiendelea na utoaji wa elimu ya mlipa Kodi na utoaji wa Risiti halali.
Wafanyabiashara wakisikiliza elimu ya mlipa kodi na utoaji wa Risiti halali.
Elimu ya mlipa kodi na utoaji Risiti halali ikiendelea kutolewa kwa Wafanyabiashara.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akiwa na Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga Faustine Mdesa na Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo wakiwa katika matembezi ya kutoa elimu ya mlipa kodi na utoaji wa Risiti halali za mauzo ya bidhaa.
Matembezi yakiendelea ya utoaji wa elimu ya mlipa Kodi kwa Wafanyabiashara na utoaji Risiti halali za mauzo ya bidhaa kwa wateja.

Matembezi yakiendelea ya utoaji wa elimu ya mlipa kodi kwa Wafanyabiashara na utoaji Risiti halali za mauzo ya bidhaa kwa wateja.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akibandika Stika kwenye baadhi ya maduka yenye ujumbe wa uwajibikaji wa kutoa na kudai Risiti halali.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akiwa na Meneja wa TRA Faustine Mdesa (kushoto) pamoja na Wafanyabiashara wakikata Keki pamoja katika kuhitimisha wiki ya huduma kwa wateja.
Muonekano wa keki.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akimlisha Keki Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga Faustine Mdessa katika kuhitimisha wiki ya huduma kwa wateja.
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga Faustine Mdessa akimlisha Keki Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi katika kuhitikisha wiki ya huduma kwa wateja.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akiendelea na zoezi la ulishaji Keki Wafanyabiashara.
Zoezi la ulishaji Keki likiendelea kwa Wafanyabiashara.
Zoezi la ulishaji Keki likiendelea kwa Wafanyabiashara.
Zoezi la ulishaji Keki likiendelea kwa Wafanyabiashara.
Zoezi la ulishaji Keki likiendelea kwa Wafanyabiashara.
Zoezi la ulishaji Keki likiendelea.
Zoezi la ulishaji Keki likiendelea kwa Wafanyabiashara.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akimmiminia Shampeni Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga Faustine Mdesa kilele cha wiki ya huduma kwa wateja.
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga Faustine Mdessa, akimmiminia Shampeni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi kuhitimisha wiki ya huduma kwa wateja.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akimmiminia Shampeni Mfanyabiashara Mkoani Shinyanga Gilitu Makula katika kilele cha kuhitimisha wiki ya huduma kwa wateja TRA.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akimimina Shampeni kwa Wafanyabiashara katika kilele cha wiki y huduma kwa wateja TRA.
Picha za pamoja zikipigwa.
Picha za Pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za Pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za Pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za Pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za Pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za Pamoja zikiendelea kupigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464