NAIBU WAZIRI KATAMBI AWAPOKEA VIJANA WA SKAUTI WALIOPELEKA UJUMBE WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MLIMA KILIMANJARO KUELEKEA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU

NAIBU WAZIRI KATAMBI AWAPOKEA VIJANA WA SKAUTI WALIOPELEKA UJUMBE WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MLIMA KILIMANJARO KUELEKEA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU

Na Mwandishi wetu, Manyara

Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu Patrobas Katambi,amewapongeza vijana wa skauti waliofanya safari ya kijasiri kupeleka ujumbe wa mbio za Mwenge wa uhuru 2023 katika kilele cha mlima Kilimanjaro Mkoani Manyara kwa ajili ya kuhitimisha mbio hizo kesho.

Mwenge wa Uhuru Kitaifa kilele chake kinahitimishwa kesho Mkoani Manyara, huku mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassani.

Maandalizi ya kuhitimisha mbio hizo za Mwenge wa Uhuru yameendelea mkoani Manyara, ambapo mapema leo Naibu Waziri Katambi amefanya matembezi ya kuwapokea vijana wa skauti waliofanya safari ya kijasiri kupeleka ujumbe wa mbio za Mwenge wa uhuru 2023 na kupatiwa Medali.

Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Shinyanga mjini, amewapongeza vijana hao wa skauti kwa kuonyesha uzalendo mkubwa na kuipenda Nchi yao

Katika mapokezi hayo Katambi alikuwa ameambatana na Waziri wa Nchi ofisi ya waziri Mkuu kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu Prof.Joyce Ndalicha pamoja na waziri wa habari,vijana, michezo na utamaduni kutoka Zanzibar Tabia Mwita

Aidha,amewaomba vijana hapa nchini waendelee kuipenda nchi yao na kuwa Wazalendo pamoja na kuunga mkono Juhudi za Rais Samia katika kuwaletea maendeleo.

Mbio za Mwenge wa Uhuru zilizinduliwa mkoani Mtwara 2/4/2023 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na zinahitimishwa kesho mkoani Manyara na kuendana sambamba na kumbukumbu ya Baba wa Taifa hayati Julius Nyerere na wiki ya vijana kitaifa.

Kauli mbiu ya mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2023 inasema' Mabadiliko ya Tabia nchi, hifadhi Mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464