DC KISHAPU AWATAKA WATUMISHI KUFUATA MIONGOZO NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAO

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe.  Joseph Modest Mkude  amewataka watumishi wa Wilaya ya Kishapu kufuata miongozo Taratibu na  Kanuni katika utekelezaji wa Majukumu yao

 

Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo jana, Octoba 2023 alipokuwa anazungumza na Watumishi katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.

"Watumishi wote tusimamie Misingi ya Kazi, kanuni za Utumishi zinaeleweka ikiwa ni pamoja na kuwahi kazini, turudini kwenye  Misingi yaani tuisimamie ifanye kazi Misingi hii isipofanya kazi tunaiuwa wenyewe kwa hiyo tusimamie misingi hii na Kanuni na tukumbushane Mara kwa Mara  na kutekeleza maelekezo ya Viongozi wa Serikali" alisema Mkude

Naye Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu  Bi.  Fatma H. Mohammed amewakumbusha Watumishi kuwa na nidhamu kazini na nje ya kazi kwaani wamebeba dhamana kubwa katika kutekeleza majukumu yao. 

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Ndugu. Emmanuel Johnson aliwasisitiza Wakuu wa Idara na Vitengo kufanya vikao vya Mara kwa Mara ili kuweza kutambuana na kuweza kushirikiana kwa urahisi katika majukumu.

Aidha  Mkuu wa Wilaya amewakumbusha watumishi kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ndiye Msimamizi Mkuu wa Watumishi wote ndani ya Wilaya.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464