WEADO WAKABIDHI MRADI WA VUNJA UKIMYA ZUIA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI WILAYA YA SHINYANGA
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
SHIRIKA la WEADO limekabidhi Rasmi Mradi wa vunja ukimya zuia mimba na ndoa za utotoni kwa jamii na halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, huku Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Simon Berege akiwataka wazazi wilayani humo kuwekeza watoto wao kwenye elimu, ambao watakuja kuwasaidia pamoja na Taifa kupata wataalamu na viongozi wa baadae.
WEADO walikuwa wakitekeleza mradi wa vunja ukimya zuia mimba na ndoa za utotoni kwenye Kata mbili za Tinde na Masengwa wilayani Shinyanga kuanzia Aprili mwaka jana na umehitimishwa Oktoba mwaka huu kwa ufadhili wa Foundation For Civil Society na wameukabidhi leo Oktoba 27, 2023.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Simoni Berege akizungumza kwenye makabidhiano ya Mradi huo, amelipongeza Shirika la WEADO kwa utekelezaji wa mradi huo kwenye Kata hizo mbili, ambao umesaidia kupunguza ukatili ndani ya jamii, huku akiwataka wazazi kuwekeza watoto wao kwenye elimu na kuacha tabia ya kuozesha watoto ndoa za utotoni, bali wawaache wasome na kutimiza ndoto zao.
"Wazazi acheni watoto wasome msiwaozeshe ndoa za utotoni, watakuja kuwasaidia baadae pamoja na Taifa kunufaika nao kwa kupata wataalamu na viongozi katika maeneo yetu," amesema Berege.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Simoni Berege.
Aidha, ametoa wito pia kwa watoto ambao wanaishi maisha duni kwamba wasijione wanyonge wanapokuwa shuleni, bali wasome kwa bidii sababu elimu haina Roho mbaya haibagui katika ufaulu, kwamba mwenye kusoma kwa bidii ndiye atakayefanikiwa katika kutimiza ndoto zake.
"Kuna usemi usemao kuzaliwa maskini siyo tatizo, tatizo ni wewe kufa maskini sababu umejitakia Mwenyewe, hivyo watoto kuzaliwa maskini siyo tatizo,someni kwa bidii msijione wanyonge shuleni mtafanikiwa katika maisha yenu na kuwa matajiri," amesema Berege.
Amesema Serikali katika Halmashauri hiyo wataendelea kushirikiana na wadau wa Maendeleo,huku akiliomba Shirika hilo la WEADO watakapokuja na mradi mwingine wapanue wigo na kwenye Kata zingine, ili kuendelea kutoa elimu kwa Jamii na kupunguza ukatili kwa watoto zikiwamo mimba na ndoa za utotoni.
Mratibu wa Mtakuwwa wilayani Shinyanga Aisha Omary, amesema bàadae ya kukabidhiwa mradi huo, wataendelea kutenga bajeti za Halmashauri ili kuendeleza mapambano ya kutokomeza ukatili zikiwamo mimba na ndoa za utotoni.
Ametaka takwimu za ndoa za utotoni za miaka mitatu kwamba zimepungua, ambapo mwaka (2020)kulikuwa na ndoa 11, (2021) ndoa 6, (2022) ndoa Moja na (2023) ndoa Moja.
Kwa upande wa mimba za utotoni mwaka jana kwa shule za msingi zilikuwa mimba 13, Sekondari 4, na mwaka huu kuanzia Januari hadi Septemba kuna mimba 5.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la WEADO Winnie Hinaya, amesema mradi huo wa vunja ukimya zuia mimba na ndoa za utotoni, wameutekeleza katika Kata hizo za Tinde na Masengwa kwa awamu ya pili,ambao ulianza mwaka jana Aprili na umehitimishwa Oktoba mwaka huu kwa ufadhili wa Foundation for Civil Society.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la WEADO Winnie Hinaya.
Amesema mradi huo wameukabidhi Rasmi kwa Jamii kupitia vikundi ambavyo walikuwa wameviunda yakiwamo Mabaraza ya watoto, Wazee, Viongozi wa dini, na Majukwaa ya Wanawake, washirikiane pia na viongozi wa Serikali na Halmashauri kuendeleza mapambano ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Simoni Berege akizungumza kwenye kikao cha makabidhiano ya mradi kutoka WEADO.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Joseph Ntomela akizungumza kwenye kikao cha makabidhiano ya mradi kutoka WEADO.
Mratibu wa Mtakuwwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omary akizungumza kwenye kikao hicho cha makabidhiano ya mradi kutoka WEADO.
Mwakilishi wa dawati la jinsia kutoka Jeshi la Polisi akizungumza kwenye kikao hicho.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la WEADO Winnie Hinaya akielezea namna walivyotekeleza mradi huo katika Kata ya Tinde na Masengwa wilayani Shinyanga.
Afisa ufuatiliaji na Tathimini kutoka WEADO John Eddy akizungumza kwenye kikao hicho.
Afisa kutoka WEADO Mary Mndeme akizungumza kwenye kikao hicho.
Mafisa kutoka Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha makabidhiano ya mradi kutoka Shirika la WEADO.
Kikao cha makabidhiano ya mradi wa vunja ukimya zuia mimba na ndoa za utotoni kutoka Shirika la WEADO kikiendelea.

Wanafunzi kutoka Mabaraza ya watoto wakiwa kwenye kikao hicho cha makabidhiano ya mradi wa vunja ukimya zuia mimba na ndoa za utotoni kutoka Shirika la WEADO.

Mwanafunzi Rose Kazimili kutoka Tinde Girls akishukuru mradi huo kwa kusaidia kupunguza matukio ya ukatili.

Wananchi wakishukuru mradi huo wa WEADO kupunguza ukatili ndani ya jamii.

Watumishi kutoka Shirika la WEADO wakiwa kwenye kikao hicho cha kukabidhi mradi.
Watumishi kutoka Shirika la WEADO wakipiga picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Simon Berege na baadhi ya watumishi wa Halmashauri hiyo.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464