JESHI LA POLISI LAKABIDHI PIKIPIKI KWA POLISI KATA SHINYANGA

 


Jeshi la Polisi nchini limekabidhi pikipiki nane kwa Polisi kata Mkoa wa Shinyanga ili kuwarahishia utendaji kazi.

Pikipiki hizo zimekabidhiwa leo Jumamosi Oktoba 28, 2023 Kamanda wa polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishna msaidizi wa Polisi ACP Janeth Magomi niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Camilius Wambura wakati akifunga mafunzo ya utayari kwa wakaguzi na wakaguzi wasaidizi 56 awamu ya nne iliyofanyika katika uwanja wa Line Polisi Kambarage Mjini Shinyanga.


Kata ambazo zilizonufaika na pikipiki hizo ni kata ya Ulowa, Kinamapula halmashauri ya Ushetu, Mwamalili , Chibe Manispaa ya Shinyanga, Kashishi , Ngaya, Kinaga, Ngofila halmashauri ya Kishapu na Didia Halmashauri ya Shinyanga.

Kwa upande wa askari kata wa liokabiziwa pikipiki wameshukuru kwa msaada huwa kwani pikipiki hizo zinakwenda kuwapunguzia adha ya usafiri ambayo walikuwa akiipata wakati wakitekeleza majukumu yao katani sasa wataongeza ufanisi katika kutekeleza majukumu yao ikiwa sambamba na kufika maeneo ya mbali katika kata na kwa wakati.

Pia Kamanda Magomi ametoa tuzo na vyeti kwa askari polisi waliofanya vizuri katika kipindi cha mwaka 2022/2023












Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464