RC MNDEME AKAGUA MAENDELEO UJENZI UWANJA WA NDEGE WA IBADAKULI SHINYANGA
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amekagua Maendeleo ya upanuzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege uliopo Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga,na kuagiza ukamilike kwa wakati ili uanze kufanya kazi.
Amefanya ziara hiyo leo Oktoba 31,2023 akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali.
Amesema ameridhika na kasi ya ujenzi wa Uwanja huo wa Ndege, na kusisitiza kasi hiyo iendelee hivyo hivyo ili ukamilike kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi wa Shinyanga, na kuwaondolea adha ya kusafiri kwenda Jijini Mwanza kupanda Ndege.
“Mradi huu ni wa miezi 18 ambao ulianza kazi Aprili mwaka huu, na utakamilika Novemba mwakani, nakuomba Mkandarasi kasi uliyonayo uendelea nayo ili ujenzi wa Uwanja huu wa Ndege ukamilike ndani ya muda uliopangwa na kuanza kutoa huduma,”amesema Mndeme.
Aidha, amemuagiza Mkandarasi huyo azingatie pia suala la kipaumbele cha ajira kwa wananchi ambao wanazunguka eneo hilo la uwanja wa Ndege, huku akimwahidi kuwa Serikali itampatia ushirikiano na pale anatapokabiliana na changamoto yoyote asisite kuwawasiliana na Ofisi ya Mkoa ili itatuliwe.
Pia Mndeme amempongeza Rais Samia kwa kutoa fedha Sh,Bilioni 52.8 kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja huo wa Ndege Mkoani Shinyanga ambao utakuwa ni chachu ya maendeleo mkoani humo na kukuza uchumi.
Naye Meneja Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Shinyanga Mhadisi Mibara Ndirimbi ambao ndiyo wasimamizi wa mradi huo, amesema ujenzi wa Uwanja huo wa Ndege kwa sasa upo asilimia 4 na wapo kwenye ujenzi wa Barabara ya Ndege (Run Way) na utakamilika kwa wakati.
Kwa upande wake Meneja Miradi wa Kampuni ya CHICO Shi Yinlei, amemuahidi Mkuu huyo wa Mkoa, kwamba ujenzi wa Uwanja huo wa Ndege wataukamilisha kwa wakati ndani ya muda wa Mkataba, na wataujenga kwa ubora zaidi sababu vifaa vyote vya ujenzi wanavyo.
Tazama picha hapa chini ujenzi Uwanjwa Ndege👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiwa katika Ziara ya kukagua Maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Ibadakuli Shinyanga.
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Mibara Ndirimbi (kushoto) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme juu ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Ibadakuli.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiendelea kusikiliza maelezo ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof; Siza Tumbo (kulia) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi katika ziara ya ukaguzi wa Uwanja wa Ndege wa Ibadakuli.
Upanuzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege Ibadakuli ukiendelea.
Upanuzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege Ibadakuli ukiendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme awali akisamiliana na Wakandari kutoka CHICO ambao wanajenga Uwanja wa Ndege Ibadakuli.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme awali akisamiliana na Wakandari kutoka CHICO ambao wanajenga Uwanja wa Ndege Ibadakuli, alipowasili kukagua Maendeleo ya ujenzi wa Uwanja huo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464