MHE. KATAMBI AZINDUA HUDUMA YA GESI KIGANJANI
Na mwandishi wetu
Dar es salaam
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amezindua huduma ya gesi kiganjani itakayo wawezesha watumiaji kununua ama kuongeza gesi kupitia mfumo wa M-pesa supper App.
Kuzinduliwa kwa huduma hiyo ni ushirikiano wa kimkakati baina ya Vodacom na Gas Fasta ambao watawafikishia gesi watumiaji kwa gharama nafuu hivyo kuwaondolea gharama za kutembea umbali mrefu kujaza gesi.
Mhe. Katambi amebainisha hayo Oktoba 23, 2023 Jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi huduma hiyo akimwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko.
Amesema huduma hiyo itarahisisha kukuza biashara, kutunza fedha inayotokana na malipo anayoyapata mteja baada ya kutumia huduma hiyo na kutoa ajira kwa watanzania.
Aidha, amesema serikali imekusudia kupunguza matumizi ya mkaa na kuni ili kulinda mazingira ambapo kufikia 2024 Taasisi zilizo na watu zaidi ya 300 zitaanza kutumia nishati mbadala ikiwemo gesi asilia.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464