RC MNDEME AMPONGEZA RAIS SAMIA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA SHINYANGA

RC MNDEME AMPONGEZA RAIS SAMIA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA SHINYANGA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme amempongeza Rais Samia kwa kuboresha huduma za kiafya mkoani Shinyanga, pamoja na kutoa vifaa tiba vya kisasa ikiwamo Digital X-Ray Mashine na CT-SCAN ya kisasa na kutoa huduma bora ya matibabu kwa Wananchi na kuokoa Afya zao.

Amebainisha hayo leo Oktoba 31, 2023 wakati alipofanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kuona utoaji wa huduma za matibabu pamoja na kuzungumza na watumishi wa hospitali hiyo.
RC Mndeme akiwa katika chumba cha CT-SCAN.

Amesema amefarijika kuona maendeleo makubwa ya utoaji wa matibabu katika Hospitali hiyo vikiwamo na vifaa tiba vya kisasa na kuwaondolea adha wananchi kufuata huduma za matibabu katika Hospitali ya Bugando Jijini Mwanza, sababu huduma zote za matibabu ya kibingwa kwa sasa zinapatikana katika Hospitali hiyo.

“Mkoa wa Shinyanga tunampongeza Rais Samia kwa kuboresha huduma za Afya hapa Shinyanga na katika Hospitali yetu ya Rufaa ametoa vifaa Tiba vya kisasa kabisa ikiwamo Digital X-Ray Mashine, na CT-SCAN, pia tuna kiwanda cha kuzalisha hewa ya Oksijeni na huduma hii hutolewa bure kwa wagonjwa, tunamshukuru sana Rais wetu kwa kujali Afya za Wananchi,”amesema Mndeme.
RC Mndeme akiwa katika chumba cha CT-SCAN.

Aidha, ameagiza vifaa hivyo tiba vitunzwe ili vitoe huduma ya matibabu kwa muda mrefu, pamoja na kudhibiti wizi wa madawa, huku akibainisha kuwa Rais Samia ameshatoa tena Magari ya wagonjwa (Ambulance) katika Halmashauri zote Sita za Mkoa huo na Hospitali ya Rufaa, na kuagiza Magari hayo yatunzwe pia.

Amewataka watumishi wa Hospitali hiyo kuendelea kutoa huduma bora ya matibabu kwa wananchi na kupunguza vifo vya uzazi, kuacha kuchati na simu za mkononi wakati wa kutoa matibabu, kujiepusha na Rushwa, kutumia lugha Rafiki kwa wagonjwa pamoja na kutoa elimu ya kujikinga na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
RC Mndeme akiwa katika chumba cha CT-SCAN.

Katika hatua nyingine amesema changamoto ambazo zimewasilishwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo zitafanyiwa kazi ikiwamo ya upungufu wa majengo, watumishi, uzio na ujenzi wa barabara kiwango cha lami kutoka Ndala hadi Hospitalini hapo.

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga DK, Luzila John amesema wanamshukuru Rais Samia kuwa kuboresha huduma za Afya katika Hospitali hiyo ikiwamo na utoaji wa Vifaa Tiba vya kisasa na wamekuwa wakitoa huduma bora ya matibabu kwa wananchi.
RC Mndeme akiwa katika chumba cha Digital X-Ray Mashine.

Amesema Hospitali inakabiliwa na upungufu wa watumishi 225, waliopo ni 259, uhitaji ni 481 lakini wameajiri watumishi wa Mkataba 98, na wanakabiliwa pia na upungufu wa Majengo 20 yaliyopo ni Matano, na kuahidi wataendelea kutoa huduma bora za matibabu licha ya kukabiliwa na mapungufu hayo.
Tanzama picha hapa chini👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiwa ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiwa ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiwa ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiwa katika chumba cha matibabu ya meno.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiwa katika kiwanda cha kuzalisha hewa ya Oksijeni.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiwa katika kiwanda cha kuzalisha hewa ya Oksijeni.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dk.Luzila John akitoa taarifa ya utoaji huduma za matibabu Hospitalini hapo.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza na baadhi ya watumishi katika Hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Watumishi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye kikao na Mkuu wa Mkoa.
Watumishi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye kikao na Mkuu wa Mkoa
Watumishi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye kikao na Mkuu wa Mkoa.
Picha ya pamoja ikipigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464