SHIRIKA LA NANCY FOUNDATION WATOA MSAADA WA FEDHA KWA AJILI YA CHAKULA SHULENI KWA WATOTO WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU


KATIKA kuadhimidha siku ya lishe nchini,Shirika la NANCY FOUNDATION lililopo Manispaa ya Shinyanga,limetoa msaada wa fedha kiasi cha shilingi laki 5 kwa ajili ya huduma ya uji na chakula shuleni,kwa wanafunzi 150 wa shule mbalimbali za msingi wanaotoka kaya zenye mazingira magumu.

Mkurugenzi wa Shirika hilo EZRA MAJERENGA,akikabidhi msaada huo leo kwa Afisa lishe manispaa ya Shinyanga AMANI MWAKIPESILE kwa niaba ya mkurugenzi wa manispaa,amesema shirika limekuwa na mradi wa kuwarudisha shule watoto wa mtaani,kuwawezesha vifaa vya shule,kuchangia huduma ya lishe kwa wanafunzi hao lengo ni kuunga mkono jitihada za serikali za kumuwezesha mtoto kusoma.
Mkurugenzi wa Shirika la NANCY FOUNDATION Ezra Majerenga (kulia) akikabidhi fedha Sh.Laki 5 kwa Afisa Lishe Manispaa ya Shinyanga Amani Mwakipesile kwa ajili ya chakula shuleni kwa watoto ambao wanaishi mazingira magumu.

Kwa upande wake Afisa lishe wa manispaa Amani Mwakipesile ,amemshukuru Mkurugenzi huyo wa NANCY FOUNDATION huku akitoa wito kwa wazazi,wadau wa elimu na mashirika mengine kuunga mkono mpango wa serikali wa kutoa chakula lishe mashuleni kwani inamsaidia mwananfunzi kujifunza vyema na pia kukabiliana na hali ya udumavu,ukondefu na utapia mlo.

Naye Afisa elimu manispaa ya Shinyanga Judith Magembe  ameeleza kuwa ufadhili wa chakula kwa wanafunzi unaotolewa na NANCY FOUNDATION,utaongeza chachu ya mwanafunzi kujifunza na kuinua ufaulu huku akisisitiza msaada huo utafika kwa walengwa ambao ni wanafunzi wanaotoka mazingira magumu.
Mhoja Samson na Happness Wasa wanafunzi wa shule ya msingi Town,wakishiriki maadhimisho ya siku ya lishe,wametoa wito kwa serikali,wazazi,mashirika na wadau wa elimu kulivalia njuga suala la chakula na lishe mashuleni,kwa kuwa linasaidia kumjengea afya bora mwanafunzi na kuongeza uwezo wa kuelewa darasani.

Maadhimisho ya siku ya lishe kitaifa,katika ngazi ya halmashauri ya manispaa ya Shinyanga,yamefanyika leo katika viwanja vya sabasabalishe yakijumuisha baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za manispaa hiyo na kauli mbiu ikiwa ni “Lishe bora kwa vijana balehe,chachu ya mafanikio yao”

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464