RC MNDEME AMEAGIZA UJENZI OFISI YA MKURUGENZI WA MASHTAKA SHINYANGA IKAMILIKE KWA WAKATI


RC Mndeme ameagiza ujenzi Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Shinyanga ikamilike kwa wakati

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme amemuagiza Mkandarasi kutoka Kampuni ya Elerai Construction kuhakikisha anakamilisha kwa wakati ujenzi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka mkoani humo.

Ametoa maagizo hayo leo Oktoba 31, 2023 wakati alipotembelea kuona Maendeleo ya ujenzi wa Ofisi hiyo ambayo kwa sasa imefikia asilimia 60.
Amesema ujenzi wa Ofisi hiyo ya Mkurugenzi wa Mashtaka ni muhimu sababu wananchi watapa huduma za msaada wa Kisheria na kudai haki zao kwa haki, na kuagiza kwamba hadi kufikia Decemba 29 Jengo hilo liwe tayari limekabidhiwa na Januari 2, 2024 Mkurugenzi wa Mashtaka aanze kufanya kazi akiwa ndani ya Ofisi hiyo mpya.

“Mkandarasi umeaminiwa fanya kazi, sababu pesa zipo na hakuna kisingizio, fanya kazi hadi siku ya Sikukuu ya Christimas tunaka Ofisi hii ianze kufanya kazi mwakani,huduma za Kisheria ni muhimu sana kwa jamii,”amesema Mndeme.
Naye Mkandarasi kutoka Kampuni ya Elerai Construction Mhandisi Hussein Msuya, akisoma taarifa ya ujenzi wa Ofisi hiyo ya Mkurugenzi wa Mashtaka, amesema ulianza mwaka jana na watakamilisha decemba mwaka huu, na gharama zake ni Sh.Bilioni 2.1 na sasa ujenzi upo asilimia 60.
Mkandarasi kutoka Kampuni ya Elerai Construction Mhandisi Hussein Msuya akisoma taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa Ofisi hiyo ya Mashtaka.
Muonekano wa Jengo la Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Shinyanga.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464