MADIWANI WALALAMA KUKITHIRI WIZI MASHULENI,WEZI WAIBA HADI MASUFURIA YA KUPIKIA CHAKULA WANAFUNZI

MADIWANI WALALAMA KUKITHIRI WIZI MASHULENI, WEZI WAIBA HADI MASUFURIA YA KUPIKIA CHAKULA WANAFUNZI

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MADIWANI wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, wamelalamikia kitendo cha kukithiri wimbi la wizi mashuleni kwa kuiba mali za shule yakiwamo na masufuria ya kupikia chakula cha wanafunzi.

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 30,2023 kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga wakati wa kuwasilisha taarifa za utendaji kazi kwenye Kata zao.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye Baraza.

Madiwani hao wakati kila mmoja akiwasilisha taarifa yake ya kwenye Kata, baadhi walilalamikia tatizo la kukithiri kwa wimbi la wizi wa mali za shule yakiwamo na masufuria ya kupikia chakula wanafunzi.

Mmoja wa Madiwani hao Hassan Mwendapole wa Kata ya Kambarage, amesema sasa hivi kumeshamili tatizo la wizi mashuleni kwa kuibwa mali za shule mara kwa mara.
Naye Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, amesema tatizo hilo la wizi Mashuleni limeshamili na hata katika shule ya Msingi Chamaguha wameiba mali za shule yakiwamo masufuria ya kupikia chakula cha wanafunzi.

"Shule ya Msingi Chamaguha napo wameiba mali za shule na masufuria ya kupikia chakula, sasa hivi watoto wanashindwa kula shuleni sababu ya vyombo vyao kuibiwa," amesema Meya Masumbuko.
Amesema hatua ambayo wataichukua Halmashauri ni kuanzisha suala la ulinzi Shirikishi maeneo yote ya shule au kutunga sheria ndogo ya kubana wazazi kuchangia pesa ya mlizi ili kulinda mali za shule, na kubainisha kwamba shule nyingi za Manispaa ya Shinyanga zipo wazi na hazina uzio ndiyo maana ni virahisi wezi kuiba.

Aidha, katika Baraza hilo ziliwasilishwa changamoto mbalimbali ambazo bado zinawakabili wananchi likiwamo suala ya ubovu wa Miundombinu ya Barabara, ukosefu wa Maji, Umeme, upimaji viwanja, upungufu matundu ya vyoo, Maghuba kukithiri uchafu, upungufu watumishi na majina kutoonekana kwenye mfumo wa CHF.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze, amesema changamoto zote ambazo zimewasilishwa kwenye Baraza hilo na Madiwani zitaendelea kutatuliwa.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani .

Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza.
Kikao cha Baraza la Madiwani kikiendelea.
Diwani wa Kizumbi Lubeni Kitinya akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Madiwani wakiendelea na kikao cha Baraza.
Diwani wa Kolandoto Mussa Andrew akizungumza kwenye kikao cha Baraza.
Madiwani wakiendelea na kikao cha Baraza.
Diwani wa Ngokolo Victor Mkwizu akizungumza kwenye kikao cha Baraza.
Kikao cha Baraza kikiendelea.
Diwani wa Kitangili Mariamu Nyangaka akizungumza kwenye kikao cha Baraza.
Madiwani wakiendelea na kikao cha Baraza.
Kikao cha Baraza kikiendelea.
Diwani wa Vitimaalumu Zuhura Waziri akiwa kwenye kikao cha Baraza akipitia nyaraka.
Diwani wa Vitimaalum Pica Chogelo akiwa kwenye kikao cha Baraza.
Kikao cha Baraza kikiendelea.
Kikao cha Baraza kikiendelea.
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464