RC MNDEME AWAELEZA WANAWAKE WA KIISLAMU MKOANI SHINYANGA MAMBO MAZURI ALIYOFANYA RAIS SAMIA MKOANI HUMO

RC MNDEME AWAELEZA WANAWAKE WA KIISLAMU MKOANI SHINYANGA MAMBO MAZURI ALIYOFANYA RAIS SAMIA MKOANI HUMO

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amekutana Jumuiya ya wanawake wa Kiislamu Mkoa wa Shinyanga, kufahamiana, kula nao chakula pamoja na kuwaeleza fedha ambazo zimetolewa na Rais Samia mkoani humo na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Amekutana na Jumuiya ya wanawake wa Kiislamu mkoani Shinyanga leo Oktoba 4, 2023 katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Mndeme akizungumza na wanawake hao, amewaomba waendelee kumuunga Mkono Rais Samia katika utawala wake ili aendelee kutafuta fedha na kuwatekelezea miradi mbalimbali ya Maendeleo, ikiwamo ya Maji na kumtua ndoo kichwani Mwanamke, Miradi ya Afya, Elimu, na Miundombinu ya Barabara.

Amesema katika Mkoa huo wa Shinyanga ndani ya Utawala wa Rais Samia ameshatoa kiasi cha fedha Sh,Trilioni 1 ambazo zimetekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, na kwamba katika Marais bora  duniani Rais Samia ni mmoja wao.

“Tunakila sababu ya kujivunia Rais Samia na tunapaswa kumuunga Mkono katika Utawala wake ili awatumikie Watanzania na kuwaletea maendeleo,”amesema Mndeme.
Aidha, akizungumzia upande wa Sekta ya Afya, amesema Rais Samia ameboresha huduma za Afya mkoani humo ikiwamo na upatikanaji wa madawa na vifaa tiba vya kisasa na kuwaomba Wanawake watumie huduma hizo za afya kupata matibabu na kuokoa Afya zao na hakuna sababu ya kupoteza maisha sababu ya uzazi sababu huduma zipo na bora zaidi.

“Hospitali yetu ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga inatoa huduma za kibingwa na Rais Samia ametuletea vifaa vya kisasa kabisa ikiwamo CT-SCAN, X-RAY,pia kaongeza Sh,bilioni moja ili kuboresha hospitali hiyo kwa kujenga ICU, Jengo la wagonjwa wa dharura, na Idiology,”amesema Mndeme.
Amesema kwa upande wa ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha Lami kutoka Kolandoto hadi Lalago tayari kiasi cha fedha Sh.bilioni 12 kimeshatengwa pamoja na ujenzi wa Barabara kutoka Kahama hadi Kakola Sh,bilioni 93.

Pia, amewaita wawekezaji kuwekeza mkoani humo ambapo tayari kuna maeneo yameshatengwa kwa ajili yao, na kubainisha kwamba kwa sasa mkoa huo una Jumla ya Viwanda 838 kutoka 730 sawa na ongezeko la Viwanda 108.
Katika hatua nyingine amewataka wanawake kuchangamkia fursa zilizopo mkoani Shinyanga ili wajikwamue kiuchumi ikiwamo kuingia kwenye shughuli za uchimbaji wa madini na kuahidi kwamba Serikali itaendelea kuwaunga mkono.

Mndeme amewataka pia akina mama kuendelea kusimamia maadili ya watoto wao, pamoja na kuwalinda dhidi ya watu ambao hufanya vitendo hivyo na kuacha pia kuwalaza pia chumba kimoja na wageni.
Katika hafla hiyo Mndeme ameahidi kutoa Mifuko 100 ya Saruji kwa ajili ya kuwaunga Mkono Jumuiya ya wanawake wa Kiislamu wilayani Kahama, ambao wapo kwenye ujenzi wa ukumbi wao huku SHUWASA nao wakiahidi kutoa Sh,200,000.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake wa Kiislamu Tanzania Mkoani Shinyanga Aisha Juma, amempongeza Mkuu wa Mkoa kwa kukutana nao na kuwaeleza mambo mazuri ya Rais Samia, huku wakiahidi kuendelea kumuunga mkono Rais kutokana na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kutatua kero zao.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu Mkoa wa Shinyanga Aisha Juma akizungumza kwenye hafla hiyo.
Maombi katika hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiswali.
Wanawake wa Kiislamu mkoani Shinyanga wakiendelea na swala.
Wanawake wa Kiislamu mkoani Shinyanga wakiendelea na swala.
Wanawake wa Kiislamu mkoani Shinyanga wakiendelea kuswali.
Wanawake wa Kiislamu mkoani Shinyanga wakiendelea kuswali.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kushoto)akiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake wa Kiislamu Mkoa wa Shinyanga Aisha Juma wakiteta jambo katika hafla hiyo.
Wanawake wa Kiislamu Mkoani Shinyanga wakiwa kwenye hafla ya Mkuu wa Mkoa.
Wanawake wa Kiislamu Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye hafla ya Mkuu wa Mkoa.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye hafla ya Mkuu wa Mkoa.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya (kulia) akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Prof; Siza Tumbo katika hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (wapili) akichukua chakula kwa ajili ya kula chakula cha pamoja na wanawake wa Kiislamu mkoani Shinnyanga na Sheikh wa Mkoa huo Ismail Mkusanya.
Zoezi la uchukuaji chakula likiendelea.
Zoezi la uchukuaji chakula likiendelea.
Zoezi la uchukuaji Chukula likiendelea.
Zoezi la uchukuaji Chukula likiendelea.
Zoezi la uchukuaji chakula likiendelea.
Zoezi la uchukuaji chakula likiendelea.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464