Wanawake Shinyanga waguswa na utawala wa Rais Samia wampatia Tuzo ya pongezi utekelezaji miradi ya Maendeleo
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
WANAWAKE katika Mkoa wa Shinyanga wamempatia Tuzo ya pongeza Rais Samia, kutokana na kutoa fedha nyingi na kutekelezwa miradi mbalimbali ya Maendeleo mkoani humo na Tanzania kwa ujumla na kila kijiji kimefikiwa na maendeleo hayo.
Tuzo hiyo imekabidhiwa leo Oktoba 30,2023 na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi kwaniaba ya Wanawake wote wa Mkoa wa Shinyanga, kwa Mkuu wa Mkoa huo Christina Mndeme ambaye atamfikishia Tuzo hiyo Rais Samia.
Samizi akizungumza wakati wa kukabidhi Tuzo hiyo, amesema wanawake wa Mkoa wa Shinyanga na Kamati nzima ya Maandalizi ya Kongamano la kumpongeza Rais Samia, wameamua kumpatia Tuzo hiyo ya pongezi Rais, kutokana na kuuletea maendeleo Mkoa wa Shinyanga na Tanzania kwa ujumla.
"Tunaikabidhi Tuzo hii ya kumpongeza Rais Samia kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambaye atamfikishia, ambayo ni ya kumpongeza Rais Samia kwa kazi kubwa ya kuleta Maendeleo mkoani Shinyanga na Tanzania kwa ujumla na vijiji vyote vimefikiwa," amesema Samizi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amewashukuru wanawake wa Mkoa huo wa Shinyanga kwa kutambua kazi kubwa ambayo anaifanya Rais Samia, katika kiwatumikia Watanzania na kuwaletea Maendeleo na hata kumpatia Tuzo ya pongezi.
"Kwenye Mkoa huu wa Shinyanga Rais Samia ametoa Mabilioni ya fedha na kutekelezwa miradi mingi ya Maendeleo, na katika Marais Bora 100 hapa duniani Rais Samia ni namba moja na nimpenda Maendeleo, na Tuzo hii ya pongezi nitamfikishia," amesema Mndeme.
Aidha, amewataka Wanawake hao katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani wasimwagushe Rais Samia, bali wachague viongozi wote ambao wanatokana na chama cha Mapinduzi (CCM),hivyo hivyo na uchaguzi Mkuu (2025)kwa kutochanganya gunzi na betri kwenye tochi.
Tazama matukio katika picha hapa chini👇
Awali Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akiongoza Wanawake wa Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kukabidhi Tuzo ya kumpongeza Rais Samia kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme ambaye atamfikishia Tuzo hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akiwa ameshika Tuzo ya kumpongeza Rais Samia kwa kuchapa kazi na kuuletea Maendeleo makubwa Mkoa wa Shinyanga na Tanzania kwa ujumla.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi (kushoto) akimkabidhi Tuzo ya kumpongeza Rais Samia Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiburudika na Wanawake wa Shinyanga katika zoezi la kumpatia Tuzo ya pongezi Rais Samia kwa kuuletea Maendeleo Mkoa wa Shinyanga na Tanzania kwa ujumla.
Burudani zikiendelea.
Burudani zikiendelea.
Burudani zikiendelea.
Burudani zikiendelea.
Burudani zikiendelea.
Burudani zikiendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akipiga picha ya pamoja na Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la kumpongeza Rais Samia.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kulia) akipiga picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kushoto) akipiga picha ya pamoja na Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Zamda Shabani.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa na wajumbe wa Kamati ya Kongamano la kumpongeza Rais Samia.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa na wajumbe wa Kamati ya Kongamano la kumpongeza Rais Samia.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa na wajumbe wa Kamati ya Kongamano la kumpongeza Rais Samia.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa na wajumbe wa Kamati ya Kongamano la kumpongeza Rais Samia.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akipiga picha ya pamoja na Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la kumpongeza Rais Samia.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464