Mkuu wa Msafara ,Kanali Hamis Ngoi akizungumza na Maofisa wa kijeshi ngazi ya Umeja,Ukanali na Luteni kutoka maitafa 10 waliofanya ziara yamafunzo ya ndani katika manispaaya Shinyanga
Suzy Luhende na Estomine Henry Shinyanga press blog
CHUO cha kijeshi cha ukamanda na unadhimu-Duluti Tanzania kilichopo chini ya Jeshi la ulinzi la Taifa kimefanya ziara ya mafunzo Mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuweza kujifunza hali ya usalama na amani inavyoweza kuchochea maendeleo ya kijami na kiuchumi.
Maofisa wa kijeshi ngazi ya Umeja,Luteli na Ukanali kutoka mataifa 10 ya Uganda,Burundi,Zambia,Rwanda,Msumbiji,ufalme Uswatini,Afrika Kusini, India na Tanzania wameshiriki mafunzo hayo leo Oktoba 9,2023 katika Manispaa ya Shinyanga, ziara hiyo iliambatana na wanafunzi,wakufunzi na wasaidizi wa utawala wa chuo hicho.
Mkuu wa Msafara, Kanali Hamis Ngoi amesema ziara ya mafunzo ya ndani (Domestic study visit) ni kujifunza kuhusu miradi ya kijamii na kiuchumi inavyoweza kuchochea na kuhuisha hali ya ulinzi na usalama na uwepo wa amani kwa ajili ya maendeleo.
"Maendeleo ya kijamii na kiuchumi hayawezi kufanikiwa vizuri ikiwa hakuna amani na usalama wa kutosha kwa serikali na raia wake na jukumu letu ni kusimamia amani kwa Taifa letu na shughuli zote zinahusiana na uwepo wa amani na usalama kwa upana" amesema Ngoi.
" Tumeamua kuja Shinyanga kwa kuwa ni Mkoa wa kimkakati na zipo rasilimali za kutosha ,lengo ni kuona namna utumiaji rasilimali unavyoweza kuleta uendelevu wa usalama na amani kwa shughuli za uchumi na kijamii,"ameongeza Ngoi.
Aidha Kanali Ngoi,amesema kuwa kauli mbiu ya chuo ni mwaka huu ni "Maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi katika uendelevu wa ulinzi na usalama" hivyo kufanya ziara ya mafunzo endelevu kila mara kwa maofisa wakuu wa kijeshi kuangalia hali ya ulinzi na usalama.
Naye mwanafunzi wa chuo hicho, Luteni Nkateko Masiuana kutoka Afrika Kusini amesema
amejifunza namna manispaa hiyo inavyokusanya mapato ya ndani kwa kushirikiana na jamii na kulete maendeleo ya kijamii, kiuchumi na usimamizi wa usalama na amani.
Pia Meja Joseph Murimi wa Tanzania amesema mafunzo yamemsaidia kuona namna suala la ulinzi na usalama hayo kwa manispaa ya Shinyanga lilivyoweza kufanikisha maendeloleo ya kijami na kiuchumi.
"Usalama ni suala mtambuka linagusa kila eneo la kisekta katika maendeleo ya Taifa na raia"
Kwa upande wake,Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Zamda Shabani amesema,manispaa ya Shinyanga inaendelea kukuwa na kufanya vizuri katika miradi ya maendeleo na lengo ni kuwa jiji.
"Tunawakaribisha makundi mbalimbali kufika na kujifunza juu ya utendaji wa manispaa yetu katika kufanikisha maendeleo mbalimbali ya manispaa amesema Zamda.
Afisa Maendeleo wa manispaa ya Shinyanga, Paschal Yelaa amesema, katika sekta ya elimu wamefanikiwa kujenga madarasa 78, mabweni 11,nyumba nne za watu na majengo 14 ya maabara.
Pia amesema manispaa hiyo imefanikiwa kutoa Sh 364 milioni kwa vikundi 26 vya wanawake,vijana na makundi maalum katika mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Mkuu wa Msafara Kanali Hamis Ngoi akizungumza
Mwanafunzi wa chuo cha Duluti Tanzania, Luteni Nkateko Masiuana -kutoka Afrika Kusini akizungumza alivyojifunza
namna manispaa ya Shinyanga inavyokusanya mapato ya ndani kwa kushirikiana na jamii na kulete maendeleo ya kijamii, kiuchumi na usimamizi wa usalama na amani.













