JESHI LA POLISI SHINYANGA LAWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA 05, HUKU LIKIKAMATA WATUHUMIWA 25 WA MAKOSA MBALIMBALI

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Janeth Magomi akionyesha bangi iliyokamatwa


Suzy Luhende, Shinyanga press blog

Jeshi la polisi Mkoani Shinyanga limewafikisha mahakamani watuhumiwa wa kesi mbalimbali na kuhukumiwa zikiwemo kesi 05 za kubaka ambazo zilihukumiwa miaka 30 jela na ya kulawiti ilihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na nyingine kuhukumiwa kifungo cha maisha jela na imefanikiwa kukamata watuhumiwa wa makosa mbalimbali.

Pia kesi moja ya kujiwasilisha mweyewe ilihukumiwa kifungo cha miezi 13 jela huku kesi moja ya wizi wa mifugo ikihukumiwa kutumikia jamii kwa mwaka mmoja, makosa sita ya wizi yalihukumiwa kifungo kati ya miaka mitano hadi sita jela.

Akitoa taarifa ya kipindi cha mwezi mmoja amesema wahalifu wa makosa mbalimbali wengine kufungwa jela miaka 30, wengine Maisha pia wamekamata vifaa mbalimbali vilivyodhaniwa kuwa vya wizi.

Aidha jeshi la polisi lilifanya misako na doria katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Shinyanga na kufanikiwa kukamata mali na vielelezo mbalimbali, yamekamatwa madawa ya binadamu ambayo yalikuwa yakiuzwa kiholela katika maduka binafsi ya madawa na vifaa tiba vya aina mbalimbali katika msako wa pamoja na TMDA, afya na afisa biashara uliojulikana kama operesheni PANGEA.

"Box 01 la sindano box 01 la mipira ya drip, box 01 la chupa za maji ya drip, box 01 la dawa mchanganyiko, box 03 za vipodozi vyenye viambata vya sumu na Box 01 la taulo za kike, vikiwemo viroba vitano vya mifuko ya Plastiki ambayo imepigwa marufuku nchini ambapo thamani yake haijajulikana"amesema Magomi.

Pia katika msako huo wamefanikiwa kukamata mirungi bunda 20, Bangi gramu 1800 lita 05 za pombe haramu ya moshi, vitu mbalimbali vilivyokuwa vinatumika katika kupiga ramli chonganishi pamoja na pikipiki 06 ambazo zilikuwa zinatumika katika uhalifu sehemu mbalimbali, ambapo jumla ya watuhumiwa 25 wanashikiliwa katika vituo mbalimbali vya polisi mkoani hapa kwa tuhuma hizo huku wengine wakiwa wameshafikishwa mahakamani na kupewa dhamana.

Magomi amesema katika operesheni za usalama barabarani barabarani na kukamata jumla ya makosa 3080 makosa ya magari yalikuwa 2331 ambapo magari 993 yalikuwa mabovu, magari 242 yalizidisha abiria na magari 260 yalikamatwa kwa mwendo kasi.

Amesema magari 179 hayakuwa na bima, magari 150 yalikamatwa kwa mwendo hatarishi, magari 28 madereva hawakufunga mikanda ya usalama, magari sita yaliendeshwa bila leseni na magari 473 yalikamatwa kwa makosa mbalimbali.

Amesema kwa upande wa pikipiki na bajaji jumla ya zilikamatwa 749 kutokuwa na leseni 178, ubovu wa pikipiki 46, kuzidisha abiria makosa 55, kutokuwa na bima 173, kuendesha pikipiki kwa njia hatarishi, makosa 60 kutokuvaa kofia ngumu, makosa 127 kutokuwa na leseni ya LATRA 31, na makosa mengineyo 79.

Aidha jeshi la polisi Mkoani Shinyanga limetoa wito kwa wananchi kufuata sheria za usalama barabarani na za nchi kwa ujumla hususan katika kipindi cha mwisho wa mwaka ili kulinda amani na utalivu uliopo.
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Shinyanga Janeth Magomi akitoa taarifa ya mwezi mmoja kwa vyombo vya habari mkoani Shinyanga
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Shinyanga Janeth Magomi akinyesha vitu vilivyokamatwa
Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Janeth Magomi akionyesha bangi iliyokamatwa
Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Janeth Magomi akionyesha pikipiki zilizokamatwa
Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Janeth Magomi akionyesha vipodozi vyenye viambata vya sumu.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464