MANISPAA YA SHINYANGA NA SHUWASA KUONDOA CHANGAMOTO YA UKOSEFU MAJI-SHULE YA MSINGI CHIBE

 MANISPAA YA SHINYANGA NA SHUWASA   KUONDOA CHANGAMOTO YA UKOSEFU MAJI-SHULE YA MSINGI CHIBE



Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akiongoza Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga

  Na mwandishi wetu.

Baraza la manispaa ya Shinyanga limeagiza Shuwasa na ofisi ya Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga kukaa pamoja kwa ajili ya kutatua hali ya ukosefu wa maji kwa wanafunzi shule ya msingi Chibe.

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga limeazimia limetoa  pendekezo hilo  ili kutatua changamoto ya ukosefu wa maji katika shule ya msingi chipi kwa takribani miaka miwili.

 Pendekezo hilo  limetolewa leo Jumanne Oktoba 31,2023 wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo wa Lewis Kalinjuna.

 Akitoa hoja katika mkutano huo, diwani wa kata ya Chibe John Peter Kisandu  alilamikia Shuwasa  kushidwa kuondoa tatizo hilo kwa muda mrefu licha ya mabaraza yaliyopita kuagiza kero hiyo kutatuliwa haraka kwa ajili ya kuepusha mlipuko wa magonjwa kwa wanafunzi.

Wanafunzi wa chibe wanapata tabu ya maji kwa ajili ya kuweza kujistiri baada ya bomba hilo kuharibiwa na shughuli za skauti walipokuwa na kambi pale chibe kwa mazoezi na toka hapo wanafunzi hawana maji ya kujistiri na matumizi mengine,Hii inaweza kuleta mlipuko wa magonjwa kwa wao kujisaidia vichakani” amesema Kisandu.

Meneja Huduma kwa wateja-SHUWASA,Masaka Kambesha ,alisema  ni kweli tatizo la maji katika shule hiyo lipo na watachukua hatua mathubuti kwa ushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi manispaa ili kuondoa adha hiyo kwa wanafunzi.

“Tunalichukua jambo hili na tukwenda kuliweka katika mpango wa kulifanyia kazi ili kusaidia wanafunzi wa shule hiyo”anasema Masaka Kambesha

Akiongoza Mkutano huo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko amesema ni tatizo hilo linapaswa kutojadiliwa tena katika baraza hilo na akumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze kujadilia kwa pamoja na Shuwasa kusaidia wanafunzi hao kupata maji kwa ajili ya kuweza kujistiri na kupusha hali ya mlipuko wa magonjwa.

“Sitapenda jambo hili kurudiwa tena kuulizwa kwa baraza lijalo kwa kuwa limeshalalamikiwa na diwani katika vikao vine vya nyuma ni wakati wa kutekeleza kwa kusaidia wanafunzi hawa.

Katika hatua nyingine madiwani hao walizungumzia kuhusu ni lini hali ya upatikanaji wa maji kwa watu walioko masekelo eneo karibu na hospitali watapata huduma ya maji licha ya hatua za kulazwa mabomba kuwa zimeshafanyika na pia waliomba kuweza kujua hatua za kisheria za kuwapa wananchi mamlaka kusimamia magati ya maji ili kuondoa sintofahamu inayosabisha ukosefu wa maji kwa wananchi  kutokana na kutoelewana baina  ya wasimamizi wa magati ya maji na shuwasa katika mikataba ya makubaliano. 

Akitoa salamu wakati wa kikao hicho, Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Ally Majeshi amewashukuru na kuwapongeza waheshimiwa Madiwani na watendaji wa halmashauri kwa namna wanavyotumia vizuri fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akiongoza Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Oktoba 31,2023 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akiongoza Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze akisoma taarifa kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga


Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Zamda Shaban akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga

Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Zamda Shaban akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze (kulia) akiteta jambo na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga ukiendelea
Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga ukiendelea
Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Ally Majeshi akitoa salamu wakati wa mkutano huo

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464