Na Kareny Masasy,Kahama
MDAU wa mchezo ambaye ni mkurugenzi wa Kahama TV Online Shija Felician amekabidhi seti moja ya jezi kwa timu ya waandishi wa habari (Shy Media Sports club ) iliyopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Felician amekabidhi jezi hizo leo tarehe 24,Oktoba,2023 kwa makamu mwenyekiti wa Shinyanga press club (SPC) Patrick Mabula na baadaye kukabidhiwa Kapteni msaidizi wa timu hiyo Pachal Malulu ambaye ni mwandishi wa habari wa redio ya Huheso Fm.
Felician amesema ameguswa kutoa jezi kwa waandishi wa habari zenye thamani ya sh 350,000 kwani michezo ni kujenga afya na kufurahi alikuwa anaona aibu timu kuazima jezi wakati wa mashindano na yuko tayari kusaidia kadri inavyowezakana kwa changamoto zinazojitokeza.
Mabula amemshukuru mkurugenzi wa kahama TV online kwa kuwapatia jezi timu ya waandishi wa habari ambao ni sehemu ya jamii na michezo inawafanya kujenga afya ya mwili na akili.
Mabula ametoa wito kwa waandishi kushiriki matamasha mbalimbali ya michezo kufanya mazoezi kwani inajenga urafiki na isibaki dhana ya kuandika pekee.
Malulu ameshukuru kupokea jezi kwani walikuwa wanaazima jezi zilizoandikwa jina la timu nyingine msaada wa jezi hizi ni mtaji mkubwa hivi sasa tuna changamoto ya ukosefu wa mpira hivyo wanaishukuru SPC na Kahama Tv online.
“Timu yetu
imeanza mwaka huu imeanza kujiimarisha
katika mchezo kwa kila timu watakayo
kutana nayo ni kupata ushindi tunaomba wadau wengine wajitokeze kusaidia timu
hiyo”amesema Malulu.
Mwandishi wa habari Neema Sawaka ameshukuru msaada wa jezi hizo nakuomba wadau wengine wajitokeze kusaidia timu hiyo iweze kufikia malengo.jw
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464