Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiongea kwenye mkutano mkuu wa sungusungu kanda ya ziwa.
Na Kareny
Masasy, Kahama
SERIKALI imelipongeza jeshi la jadi (sungusungu) kuwa wazalendo kwenye ulinzi na usalama nakutakiwa kuendelea kushiriki katika kulinda miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali maeneo yote.
Hayo yamesemwa leo tarehe 18,Septemba,2023 na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa walinzi wa jadi kwa kanda ya ziwa uliojumuisha mikoa mitatu ya Simiyu ,Mwanza na Shinyanga nakufanyika katika kijiji cha Busanga wilayani Kahama.
Mndeme amesema jeshi la jadi liendelee kulinda amani iliyopo ili isipotee na kuwaepuka watu wenye nia mbaya na kupinga vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.
“Wito wangu kwa jeshi hili ni kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia sheria ,kanuni na taratibu za nchi ikiwa serikali itaendelea kutatua changamoto zenu”amesema Mndeme.
Mndeme amewataka waendelee kutatua changamoto zao kwa utaratibu waliojiwekea nakufikia maridhiano pia nawaagiza viongozi wote kuanzia ngazi ya wilaya ,tarafa,kata na vijiji kutoa ushirikiano kwa walinzi wa jadi kwani wanamchango mkubwa kwenye suala la ulinzi na usalama.
Mndeme amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika mkoa wa Shinyanga imeleta sh Trioni moja kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na uendeshaji katika sekta mbalimbali.
“Katika sekta ya elimu mkoa umepokea zaidi ya sh Bilioni 53.6 na sekta ya maji zaidi ya sh Bilioni 102.2 kwaajili ya utekelezaji miradi ya 47 ya maji kwenye wilaya za Kishapu miradi kumi,Kahama miradi 20 na Shinyanga miradi 17”amesema Mndeme..
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi amesema jeshi la jadi limesaidia katika ulinzi na usalama kwani polisi ni wachache na sasa kuna kampeni ya kila kata kwaajili ya kukomesha uhalifu na polisi hivi sasa wanafanya kazi kwa weledi waendelee kushirikiana kufichua wahalifu.
Mlezi, mratibu na mshauri wa sungusungu Taifa Idd Ali amesema jeshi hilo lilikuwepo lakini likafa kutokana na wao kuogopa kuonewa,kunyanyaswa na kubambikiwa kesi lakini sasa Rais Samia Suluhu amelifufua tena na kulipa uimara wako tayari kulinda amani.
Mshauri huyo kwenye mkutano huo alimtaja Charles Masanganya kuwa kamanda wa sungusungu mkoa wa Shinyanga na Tito Okuku kuwa mshauri wa sungusungu mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti
wa sungusungu kanda ya ziwa kutoka mikoa
mitano ya Shinyanga,Simiyu,Tabora,Geita na Mwanza Shimbi Morgani Martin amesema wako tayari
kulinda fedha na miradi ya wananchi akitokea kiongozi wa sungusungu kaenda
kinyume kwa kula fedha awajibishwe na kuvuliwa madaraka.
Kamanda mkuu wa sungusungu kwa mkoa wa Shinyanga John Kadama akiongea kwenye mkutano.
Jeshi la jadi wakiingia uwanjani kwa nyimbo na furaha
Mwakilishi wa waganga wa tiba za asili kanda ya ziwa Mayunga Kidoyayi
Jeshi la jadi likisikiliza viongozi kwenye mkutano.
Mwakilishi wa waganga wa Tiba za asili kanda ya ziwa Mayunga Kidoyayi.
Mwenyekiti wa sungusungu wilaya ya Kahama Kizimbu Lugomba.
Mwenyekiti wa sungusungu kanda ya ziwa Shimbi Morgani.
Tito Okuku na Charles Masanyaga wakiteuliwa kuwa viongozi wa sungusungu mkoa wa Shinyanga.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi.
Mlezi na mratibu wa mshauri wa sungusungu taifa Idd ali Ame.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita akiongea kwenye mkutano mkuu wa sungusungu.